20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

KHAN AONGOZA UCHAGUZI PAKISTANI

ISLAMABAD, PAKISTANI


CHAMA cha nyota wa zamani wa mchezo wa kriketi, Imran Khan kinaongoza matokeo ya uchaguzi mkuu nchini hapa huku zoezi la kuhesabu kura lililocheleweshwa likizua ghasia na madai ya udanganyifu.

Vyombo vya habari vya Pakstani  jana viliripoti kuwa wafuasi wa chama cha Tehreek-e-Insaf (PTI) walionekana wakishangilia ushindi wa mgombea wao ingawa ni asilimia 48 tu ya kura ambayo tayari imehesabiwa hadi sasa, kutokana na kuchelewa kuhesabu kura.

Tume ya Uchaguzi ya Pakistani (ECP) imesema mchakato wa kuhesabu kura umecheleweshwa kwa sababu za kiufundi huku ikikataa madai ya kuwapo  udanganyifu.

Katibu wa tume hiyo, Babar Yakoob amekaririwa na vyombo vya habari kuchelewa huko kumetokana na kuharibika kwa mfumo wa utoaji matokeo wa (RTS).

Kwamba programu ya simu ya mkononi iliyoanza kutumika mara ya kwanza katika uchaguzi huo ili kuhesabu kura na kutoa matokeo kutoka zaidi ya vituo 85,000 vya kupiga kura.

Katika juhudi za kutaka kutuliza ghasia zilizozuka, Yakoob alijaribu kuidhibiti hali kwa kusema tume yake itatangaza chochote kile kitakachoendelea.

“Mara moja nimekuja hapa kulishuhudia mwenyewe suala hili muhimu, ili kusitokee mjadala wowote bila sababu muhimu. Baadae kutakuwa na maendeleo zaidi juu ya suala hili,” alisema Yakoob.

Masaa machache baada ya zoezi la kupiga kura kukamilika juzi Jumatano, vyama vikuu vya kisiasa nchini humo vilidai uchaguzi ulikuwa na udanganyifu kabla ya hata matokeo kuanza kutangazwa. ]

Chama cha waziri mkuu wa zamani aliyefungwa jela Nawaz Sharif, kimelishutumu jeshi la nchi kuhusika katika udanganyifu huo.

Kwa mujibu wa matokeo yasiyo rasmi, PTI ambacho kinadaiwa kuungwa mkono na jeshi, kimepata asilimia kubwa ya kura huku cha Sharif kikishika nafasi ya pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles