26.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Kesi ya Wema Sepetu kusikilizwa tena Desemba 12

 Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Upelelezi wa kesi ya kuchapisha picha za ngono na kuzisambaza kwenye mtandao ya kijamii inayomkabili msanii Wema Sepetu haujajamilika.

Hayo yamebainika leo Jumatano Novemba 21 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde.

Wakili wa Serikali, Jenipher Masue akiiwakilisha Jamhuri amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Baada ya Wakili Masue kudai hayo, mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu kwa ajili ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Wema anakabiliwa na kosa moja la kuchapisha picha za ngono na kuzisambaza katika akaunti yake ya Instagram.

Amedai kuwa Oktoba 15, mwaka huu katika sehemu tofauti za jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kuisambaza katika akaunti yake Instagram.

Hata hivyo Wema yupo nje kwa dhamana lakini amepewa masharti ya kutoweka video za ngono na maneno yenye muelekeo wa jambo hilo katika akaunti yake hiyo.

 

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,509FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles