25 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya wanakwaya walioshtaki kanisa kusuluhishwa

ERICK MUGISHA – DAR ES SALAAM

Upande wa Jamuhuri katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es salaam umesema jalada la kesi inayowakabili wanakwaya wa kanisa la kisabato lilipo kinondoni (SDA)dhidi ya Uongozi wa kanisa hilo limepelekwa kwa Hakimu Mfawidhi kwa kupanga Hakimu wa kutoa usuluhisho.

Hakimu Esther Mwakalinga ametoa uamuzi huo wa kufunga jalada na kupelekwa kwa hakimu mfawidhi wakati kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena tarehe husika.

“Jalada la kesi hii litapelekwa kwa hakimu mfawidhi kwa ajili ya kuteua hakimu mwingine wa kuendesha kesi hiyo na kutoa suluhisho Desemba 27 mwaka huu”, amesema Hakimu Mwakalinga.

Katika kesi ya msingi wanakwaya wa kanisa la kisabato Barnas Katikiro na David Maiba wameishtaki bodi ya wadhamini wa Kanisa la Kisabato lilipo Kinondoni, Mchungaji wa kanisa hilo Masunya Antory na Joseph Mgwabi.

Wanakwaya hao walilalamika kwa uongozi wa kanisa hilo kuwa wamewatumia waimbaji wengine kufanya mkanda wa video wakati watu hao hawakuingiza sauti katika mkanda huo.

Aidha wanakwaya hao wanalalamikia kuwepo kwa mkanganyiko wa katiba ya kwaya na kudai kuwa Mahakama ina mamlaka ya kudhibitisha kuwepo kwa jambo hilo.

Kutokana na malalamiko ya wanakwaya hao walifungua kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni dhidi ya viongozi wa kanisa hilo hata hivyo viongozi hao waliweka pingamizi lenye hoja tatu zilizotaka kesi hiyo itupuliwe mbali.

Novemba 27 mwaka huu pingamizi hilo lilisikilizwa na mahakama  ambapo lilitupiliwa mbali na kupanga kesi hiyo kusikilizwa na  kutoa suluhisho Desemba 27 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles