32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Wakenya kusikilizwa Arusha

Na Mtua Salira, EANA

KESI ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha inayowakabili raia wa Kenya waliotiwa mbaroni nchini Msumbiji na kuhamishiwa Tanzania miaka tisa iliyopita, itasikilizwa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) Arusha Mei, 21, 2015.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mahakama hiyo mjini hapa jana, ilisema kesi hiyo ijulikanayo kama Onyango na wenzake tisa, wanadaiwa kutenda makosa hayo mjini Moshi na itasikilizwa kwa siku moja.
Wakenya hao wanadai katika maombi yao kwamba walikuwa nchini Msumbiji kwa ajili ya shughuli zao za kutafuta fursa za biashara, lakini walitekwa kinyume cha sheria na kuingizwa kwenye ndege ya kijeshi na kurejeshwa Tanzania, Januari 16, 2006 kisha kushtakiwa kwa mauaji na mashtaka mengine matatu ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Pia mahakama hiyo itasikiliza maombi ya Mtanzania Mohamed Abubakari, anayepinga adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kutiwa hatiani kwa mashtaka mawili ya unyang’anyi wa kutumia silaha na Mahakama ya Wilaya ya Moshi, Julai, 1998. Maombi hayo yatasikilizwa Mei 22, 2015.

Kesi hizo zitasikilizwa hadharani katika ukumbi wa Kibo, makao makuu ya AfHCPR yaliyopo kwenye jengo la ofisi za Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), eneo la Burka.
Mahakama hiyo itafanya kikao chake cha 37 cha kawaida kuanzia leo hadi Juni 5, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles