30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Kesi ya utapeli ya Masunga yapigwa kalenda

KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

Kesi ya Abdallah Bulembo ya kudaiwa kutapeliwa Sh milioni 100 inayomkabili  aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa UWT-CCM Wilaya ya Kinondoni, Frolence Masunga (45) imepigwa kalenda hadi Machi 25 mwaka huu.

Kesi hiyo inayomkabili mshtakiwa huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, mkazi wa Kimara Suka ilitajwa juzi katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala mbele ya Hàkimu Mfawidhi Martha Mpanze.

Shauri hilo linatajwa kwa mara ya pili ambapo ilishatajwa kwa mara ya kwanza Januari 22.

Masunga anashtakiwa kwa kosa la kuchukua fedha za Abdallah Majora Bulembo, kwa njia ya udanganyifu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka inadaiwa kuwa Februari mwaka jana katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es Salaam Masunga alipokea kiasi cha fedha za kitanzania Sh milioni 100 kutoka kwa Bulembo akidai anamuuzia nyumba iliyopo Kinyerezi ndani ya Manispaa ya ilala.

Mshtakiwa anadaiwa alifanya hivyo wakati akijua si kweli  kwani hakuweza kukabidhi nyaraka za nyumba hiyo kwa Bulembo hivyo nyumba hiyo kuendelea kubaki mikononi mwake.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles