25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA TIDO KUANZA KUSIKILIZWA MFULULIZO KUANZIA APRILI 24

NA KULWA MZEE -DAR EA SALAAM


KESI ya kutumia madaraka vibaya inayomkabili Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando, inatarajia kuanza kusikilizwa mfululizo Aprili mwaka huu.

Kesi hiyo iliyokuwa inasikilizwa mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa, imehamishiwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi na jana ilikuja kwa kuanza kusikilizwa.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Leonard Swai, aliomba tarehe nyingine kuleta mashahidi.

Hakimu Shaidi alisema mahakama itasikiliza kesi hiyo mfululizo siku mbili; Aprili 24 na 25, hivyo Jamhuri wanatakiwa kuita mashahidi wa kutosha.

Awali akisomewa maelezo ya awali, Tido alikubali maelezo yake binafsi.

Alikubali alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC mwaka 2006 hadi 2010.

Mshtakiwa huyo alikubali alikuwa msimamizi katika shughuli za TBC, lakini si zote.

Alikubali kutoa maelezo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), lakini alikana mashtaka yote yanayomkabili.

Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh milioni 887.1.

Inadaiwa Juni 16, 2008 akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC, kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1).

Anadaiwa kusaini mkataba huo bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BV1.

Katika shtaka la pili, Tido anadaiwa kutumia vibaya madaraka yake Juni 20, 2008 aliposaini makubaliano kwa utangazaji wa digitali duniani kati ya TBC na BV1.

Katika shtaka la tatu, anadaiwa Agosti 11, 2008 na Septemba 2008 akiwa Dubai, alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kwa ununuzi, kufunga vifaa vya usambazaji na mnara wa utangazaji kati ya TBC na BV1 na kuifaidisha BV1.

Katika shtaka la nne, anadaiwa kuwa Novemba 16, 2008 akiwa Dubai, alitumia vibaya madaraka yake kusaini mkataba wa makubaliano kuendesha miundombinu ya utangazaji (DTT Broadcast Infrastructure) kati ya TBC na BV1 na kuinufaisha BV1.

Katika shtaka la mwisho, anadaiwa kati ya Juni 16 na Novemba 16, 2008 akiwa UAE, aliisababishia TBC hasara ya Sh 887,122,219.19.

Tido anatetewa na Wakili Ramadhani Maleta na yupo nje kwa dhamana

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles