31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KESI YA SCORPION YAPIGWA KALENDA

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM


KESI ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete, maarufu ‘Scorpion’, imeahirishwa hadi Mei 2 mwaka huu, kufuatia shahidi namba nane kwenye kesi hiyo kushindwa kufika mahakamani.

Kesi hiyo iliahirishwa jana na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Flora Haule, kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali, Cheses Gavyiole, baada ya Deus Magosa (45), ambaye ni shahidi wa nane upande wa Jamhuri katika kesi hiyo ya kumjeruhi, kumtoboa Saidi Mrisho kushindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya shinikizo la damu na sukari.

Magosa ni Mkuu wa Ulinzi Shirikishi wa Baa ya Kimboka, iliyoko eneo la Buguruni, jijini Dar es Salaam, ambapo akitoa ushahidi wake Aprili 4 mwaka huu mahakamani hapo, alidai kuwa anakumbuka alitoa maelezo Polisi, lakini si hayo yaliyotolewa mahakamani.

Shahidi huyo alidai alihojiwa mara mbili ambapo ile ya kwanza ndiyo alisema ukweli ambayo haipo mahakamani na ya pili alilazimishwa akubali kusema kwamba Njwete (Scorpion) amemjeruhi mtu kwa kumtoa macho.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, alimsomea maelezo hayo ambapo kuna baadhi alikiri kuyatoa Polisi na mengine kukana na kudai kwamba askari huyo alimchukulia maelezo mara mbili, hatua ambayo iliilazimu mahakama hiyo kuahirisha kusikiliza ushahidi huo hadi Aprili 18 (jana).

Katika hati hiyo ya mashtaka, ilidaiwa kuwa, Septemba 6, mwaka huu saa 4 usiku maeneo ya Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, Njwete aliiba cheni ya silva yenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000 na black bendi ya mkononi pamoja na fedha taslimu Sh 330,000, vyote vikiwa na thamani ya Sh 474,000, mali ya Said Mrisho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles