28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

KESI YA ‘SCORPION’: DAKTARI ASEMA MAJERUHI ALITOBOLEWA UTUMBO

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM

SHAHIDI wa tano katika kesi ya unyang’anyi kwa kutumia silaha na kujeruhi inayomkabili Salum Njwete, maarufu kwa jina la ‘Scopion’, Daktari wa kitengo cha upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk. Amini Abdulrahman jana aliiambia Mahakama ya Ilala kuwa, shahidi namba moja, Saidi Mrisho alifikishwa hospitali hapo akiwa ametobolewa utumbo mwembamba.

Dk. Abdulrahmani ambaye alikuwa akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Flora Haule, alidai kuwa Septemba 7, mwaka jana, majira ya  saa 12 alfajiri akiwa chumba cha upasuaji, alipigiwa simu kutoka kitengo cha dharura cha  MNH iliyomtaka kwenda kumhudumia mgonjwa wa dharura.

Shahidi alidai kuwa alikwenda na Mrisho akiwa na majeraha mgongoni, tumboni na pia alikuwa damu machoni.

“Baada ya kumfanyia uchunguzi niligundua anahitaji kufanyiwa upasuaji kwa sababu ya jeraha kubwa lililokuwa kushoto mwa tumbo lake ambalo lilionekana lina kina kirefu na mengine madogo ambayo yalishonwa na kitengo katika dharura,” alidai Dk. Abdulrahman.

Aendelea kudai kuwa Mrisho alipelekwa chumba cha upasuaji kwa uchunguzi ambao uligundua kuwa urefu wa jeraha alilokuwanalo tumboni ni sentimita 30 kutoka katika ngozi ya ndani ya tumbo na lililotoboa utumbo mwembamba.

“Kama tundu lililokuwa katika utumbo huo lisingezibwa lingesababisha vitu vilivyomo katika utumbo huo kikiwamo chakula kuvuja nje ya mfumo wa chakula na kuingia sehemu zisizohusika hali hiyo ingesababisha kifo kwa mgonjwa.

“Nilifungua tumbo na kuliziba tundu hilo kisha nikafunga tumbo na kumpeleka wodi namba 13 na kumpa rufaa kwa wataalamu wa macho kuendelea na uchunguzi wa majeraha yake ya machoni,” alidai Dk. Abdulrahman.

Shahidi namba sita katika kesi hiyo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Muhimbili, Dk. Melida Makiya yeye alidai mahakamani hapo kuwa ndiye aliyejaza fomu ya polisi (PF3) iliyoachwa hospitali hapo na Mrisho baada ya kutibiwa na kuruhusiwa.

Dk. Makiya alidai kuwa askari mmoja alirudi baadaye kuchukua PF 3 na kukuta Dk. Abdulrahman hayupo kazini kwa sababu ya ugonjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles