28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya mita 200 kuanza leo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo linatarajia kuanza kusikiliza kesi ya kikatiba kuhusu haki ya mpigakura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au la.

Jopo hilo la majaji Seleman Kihiyo, Aliyisius Mujuluzi na Lugano Mwandambo, liliteuliwa baada ya mgombea ubunge wa Viti Maalumu Jimbo la Kilombero kupitia Chadema, Amy Kibatala, kufungua kesi hiyo kupitia kwa wakili Peter Kibatala.

Katika maombi yake, anaomba Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam itoe tafsiri sahihi ya kifungu cha 104 (1) cha sheria ya uchaguzi kuhusu haki ya mpigakura.

Mdai anaiomba mahakama hiyo iseme kwa mujibu wa kifungu hicho, wananchi baada ya kupiga kura wanaruhusiwa kukaa kwa utulivu umbali wa mita 200 au la.

Wakili Kibatala, alifungua kesi hiyo chini ya hati ya dharura katika Masjala Kuu ya Mahakama Kuu dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Amy aliyejitambulisha kama mpigakura mwenye masilahi na uchaguzi, anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu hicho sura ya 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010.

Anaiomba mahakama itafsiri kuhusu haki hiyo kwa wananchi, kwamba ni sahihi kwa wale wasiofanya kampeni kukaa umbali wa mita hizo au la.

Pia, anaiomba mahakama iiamuru NEC kutamka kwamba huo ni uvunjifu wa kikatiba kwa kuwazuia na kuwatishia wananchi kwamba watakiona cha moto.

Kifungu cha 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 kinasema: “Hakuna mtu atakayefanya mkutano siku ya kupiga kura katika au ndani ya jengo lolote ambamo upigaji kura katika uchaguzi unaendelea, au mahali popote ndani ya eneo la mita 200 ya jengo hilo, kuvaa au kuonyesha kadi ya picha yoyote, upendeleo au nembo nyingine inayoonyesha kuunga mkono mgombea fulani katika uchaguzi.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles