24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Mdee kutajwa Oktoba 7

NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

KESI ya uchochezi inayomkabili mgombea ubunge Jimbo la Kawe, Halima Mdee (Chadema) inatarajiwa kutajwa Oktoba 7.

Kesi hiyo iliyokuja jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa ajili ya mshtakiwa kujitetea, haikuendelea kwa sababu mwendesha mashtaka hakuwepo.

Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa wakili huyo ana udhuru hivyo aliomba kesi iahirishwe.

Hàkimu Simba alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 7, kwa ajili ya kutajwa.

Februari 20, mwaka huu, upande wa Jamhuri katika kesi hiyo  ya uchochezi  ulifunga ushahidi ukiwa na mashahidi watatu.

Awali Mdee alitakiwa kuanza kujitetea Julai 28, mwaka huu dhidi ya mashtaka ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli, lakini mahakama haijaanza kusikiliza utetezi.

Mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais  Magufuli.

Katika kesi hiyo, inadaiwa  Julai 3, 2017  makao makuu ya ofisi ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa ‘anaongea ovyo ovyo, anatakiwa afungwe breki’ na kwamba yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.  

 Mdee alifikishwa mahakamani hapo Julai 10, 2017 na yupo nje kwa dhamana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles