25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

KESI YA MAUAJI YA DADA WA BILIONEA MSUYA YAFUTWA

 

 

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru mke wa bilionea ErastoMsuya, Miriam Msuya na mwenzake baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kugoma kuifanyia mabadiliko hati ya mashtaka pamoja na kupewa siku tatu za kufanya hivyo.

Hakimu Mwambapa aliamua kuwaachia huru Miriam na Revocatus Muyela wanaoshtakiwa kumuua kwa kukusudia dada wa bilionea huyo, Aneth Msuya Mei mwaka jana maeneo ya Kibada Kigamboni, jijini Dar es Salaam, kwa kuwa hakuna hati inayowafanya washikiliwe kwa sababu iliyopo imebainika kuwa ni mbovu.

Hakimu Godfrey Mwambapa ameifuta kesi hiyo baada ya upande wa jamhuri kushindwa kuifanyia marekebisho hati ya mashataka ambayo ilibainika kuwa ni mbovu.

Wakili wa serikali, Hellen Moshi alidai ofisi ya DPP haiwezi kubadilisha hati hiyo sababu iko sahihi kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alidai jamhuri wamekaidi amri ya mahakama hivyo wateja wake waachiwe huru kwani hakuna hati ya mashtaka inayowashikilia.

Washtakiwa waliachiwa huru lakini walichukuliwa tena na polisi kuelekea kituoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles