26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Kesi ya mauaji Kinondoni yahamishiwa Mahakama Kuu

ERICK MUGISHA (DSJ)-DAR ES SALAAM

KESI ya mauaji inayomkabili Mustafa Ambanja mkazi wa Kigogo Kati, imehamishiwa Mahaka Kuu Kkutoka Mahaka ya Wilaya ya Kinondoni baada ya upelelezi wake kukamilika.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Matarasa Hamisi alisema November 10, 2015 eneo la Kigogo Kati Wilaya Kinondoni Dar es salaam mtuhumiwa alimuua Maulidi Shabani.

“Upelelezi wa shauri hili umekamilika kwa kuwa na Mashahidi saba,” alisema.

Alitaja mashahidi hao kuwa ni Maliki Kipesari (21) mkazi wa Kigogo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Kigogo,  Mawazo Mazoe  mkazi wa Kigogo Kati, Salimu Abdallah, mkazi wa Tageta na Safina Hamisi ambaye ni mkazi wa Mbuyuni.

Wengine alisema ni askari wa idara ya upelelezi vituo cha Morogoro Mjini na Magomeni pamoja na na vielelezo vitatu ambavyo ni ramani ya tukio, ripoti ya marehemu na maelezo ya onyo ya Mustafa Ambanja.

Hakimu Anifa Mwingira, alisema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote mpaka kesi itakapo kwenda kusikilizwa Mahakama Kuu.

“Nafunga jalada lako hapa mahakamani na kulihamishia kwenda Mahakama Kuu na utapangiwa na Msajili wa Mahakama.. Una Uhuru wa kuchagua idadi ya mashahidi unaowahitaji na kuwekewa wakili kwa upande wa utetezi ambaye atalipwa na Serikali,” alisema Hakimu Mwingira.

Mshitakiwa amerudishwa rumande mpaka kesi yake itakapo taja Mahakama Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles