30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya mauaji iliyofutwa Kisutu, yaanza upya Kinondoni

ERICK MUGISHA (DSJ)-DAR ES SALAAM 

WATUHUMIWA watatu wa mauaji ambao kesi yao ilifutwa na Mahakama ya Kisutu, wamefunguliwa mashtaka mapya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.

Watuhumiwa hao ni Mussa Akuti (30), mkazi wa Mbagala Charambe, Amon Joram (36), mkazi wa Buza Kanisani na Joseph Chamageu (32), mkazi wa Kimara Bonyokwa.

Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Hilda Katu, akiwasomea hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Anifa Mwingira, alidai Julai 8, 2015 maeneo ya Msasani kwa Mwalimu karibu na makutano ya Mwai Kibaki na Rose Garden Wilaya ya Kinondoni, washtakiwa walimuua Charles Patrick.

Hakimu Mwingira alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu chochote hadi kesi hiyo itakapokwenda Mahakama Kuu.

Mshtakiwa Amon aliomba mahakama iwaandikie kumbukumbu ya kesi yao ndani ya jalada la kesi inayowakabili.

“Mheshimia tunaomba utuandikie kumbukumbu ya kesi yetu ya awali katika jalada hili jipya maana kesi imekuja kufunguliwa kwa mara ya pili.

“Kesi hii ilishasikilizwa Mahakama ya Kisutu na tuliachiwa huru mbele ya Mheshimiwa Pamela Mazengo na tunaomba turudishwe gereza la keko,” alisema mshtakiwa Amon.

Hakimu Mwingira alisema watuhumiwa watarudishwa gereza la Keko na kesi yao itatajwa jena Julai 31.

Wakati huo huo, mkazi wa Mwananyamala, Issa Hamisi (27), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kinondoni kwa kosa la wizi wa kutumia silaha.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Veronica Mtafya, akimsomea shtaka lake mbele ya Hakimu Boniface Lihamwike, alidai Januari  17 mwaka 2018 maeneo ya Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni, aliiba simu aina ya Samsung S8 yenye thamani ya Sh milioni 1.7 mali ya Juliana Handri na kabla na baada ya tukio walimtishia kwa kwa panga na kisu.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na hakimu alisema kesi hiyo haina dhamana na itasomwa tena Julai 30.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles