Kesi ya kupinga ushindi wa Rais Lungu yatupwa

0
973
Edgar Lungu
Edgar Lungu
Edgar Lungu

LUSAKA, ZAMBIA

MAHAKAMA ya Katiba nchini Zambia imetupilia mbali kesi ya mgombea urais wa chama cha upinzani cha United Party for National Development (UPND), Hakainde Hichilema dhidi ya ushindi wa Rais Edgar Lungu.

Katika uamuzi wa wengi, jopo la majaji katika mahakama hiyo liliamua kuwa muda wa mwisho uliowekwa kusikiliza kesi hiyo ulikuwa umekwisha.

Lungu alitetea kiti chake baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 50 ya kura katika uchaguzi uliofanyika Agosti 11, mwaka huu.

Lakini Hichilema alipinga matokeo hayo na kuwasilisha ombi la kuyapinga Agosti 19.

Sheria inasema mahakama ya kikatiba ina siku 14 kusikiliza kesi hiyo.

Lakini muda huo ulikumbwa na mabishano na ilipofika Ijumaa, mawakili wa Hichilema waliondoka mahakamani wakidai ukosefu wa muda.

Hivyo, mahakama hiyo iliendelea mapema jana na kutangaza uamuzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here