27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi ya Kabendera yapigwa kalenda

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili  Mwandishii Erick Kabendera ,   imeahirishwa hadi Novemba 7 mwaka huu na hakuna taarifa iliyotolewa na Jamhuri kuhusu majadiliano waliyoanza kufanya na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) ya namna ya kumaliza kesi inayowakabili.

Hayo yalibainishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam  mbele ya Hakimu Mkazi Vicki Mwikambo wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele yake kwa sababu Hakimu anayesikiliza shauri hilo, Augustine Rwizile hakuwepo.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika, aliomba kuahirisha hadi tarehe nyingine.

Mahakama ilikubali kuahirisha hadi Novemba 7, mwaka huu na mshtakiwa alirudishwa rumande.

Hivi karibuni Wakili wa utetezi Jebra Kambole aliijulisha Mahakama kwamba mteja wake aliandika barua  kwa mujibu wa kifungu namba 194A(2) cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama ilivyofanyiwa mareje mwaka 2019. Hata hivyo hakukuw a na majibu yoyote kuhusu barua hiyo.

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173.

Katika shtaka la kwanza ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, Kabendera alijihusisha  na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili ilidaiwa katika kipindi hicho,bila ya sababu,alikwepa kodi ya sh. 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Shtaka la tatu, kabendera anadaiwa kutakaisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles