28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Kesi ya Kabendera kuendelea leo

Kulwa Mzee – Dar es Salaam

KESI ya uhujumu uchumi inayomkabili, mwandishi  wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera, imeahirishwa kwa saa 24 hadi leo kwa kutajwa.

Kesi hiyo ilikuwa inatajwa jana katika Mahakama ya Hàkimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Janeth Mtega na kuahirishwa hadi leo.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka akiiwakilisha Jamhuri, alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, akaomba iahirishwe hadi leo.

Januari 27, mwaka huu wakati kesi hiyo inatajwa, upande wa Jamhuri ulidai majadiliano na Mkurugenzi wa Mashtaka  nchini (DPP) ya jinsi ya kumaliza kesi hiyo yanaendelea.

Kabendera anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka matatu likiwamo la utakatishaji wa zaidi ya Sh milioni 173.

Katika shtaka la kwanza, inadaiwa kati ya Januari, 2015 na Julai 2019 alijihusisha na mtandao wa kihalifu kwa kutoa msaada kwa genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Shtaka la pili ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho, bila ya sababu, alikwepa kodi ya Sh 173,247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika shtaka la tatu, Kabendera anadaiwa kutakatisha Sh 173,247047.02 huku akijua fedha hizo ni mazalia ya kosa la kujihusisha na genge la uhalifu na utakatishaji fedha.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles