KESI YA BARLOW KUANZA TENA KESHO

0
517

Na MASYENENE DAMIAN


KESI ya mauaji  ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow  inayowakabili watuhumiwa saba   inatarajiwa kuendelea kusikilizwa  kesho  katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza mbele ya Jaji Sirilius Matupa.

Kesi hiyo inaendelea baada ya kusimama kwa takribani   mwaka mmoja tangu Machi mwaka jana kutokana na kukosa bajeti ya kuiendesha.

Ilisimama ikiwa imefikia hatua ya washitakiwa kuanza kutoa utetezi wao.

Kwa Mujibu wa Msajili wa Mahakama hiyo, Fransic Kabwe, kesi hiyo itaanza kuunguruma Aprili 27  mwaka huu mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Sirilius Matupa baada ya kupata bajeti ambako  mawakili wa serikali wanaongozwa na Robert Kidando, Ajuae Bilishanga na Revina Tibilengwa.

Watuhumiwa katika  kesi hiyo  ni Muganyizi Peter, Chacha Mwita, Magige Mwita, Bughanzi Edward, Bhoke Marwa, Abdalah Petro na Abdulahman Ismail.

Wanashitakiwa kumuua kwa kukusudia Kamanda Barlow kwa kumpiga risasi eneo la Kitangiri Oktoba 13,  2012 ambaye alifariki  dunia papo hapo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here