30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

KESI YA ASKOFU MOKIWA KUMALIZWA NJE YA MAHAKAMA

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imebariki aliyekuwa Askofu wa Anglikana Jimbo la Dar es Salaam Valentino Mokiwa, Askofu Mkuu wa Makanisa ya Anglikana Tanzania Mhashamu Dk. Jacob Chimeledya na Bodi ya Wadhamini ya kanisa hilo wakamalize mgogoro wao katika nyumba ya maaskofu.

Uamuzi huo wa mahakamaka ulitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya wakili wa Askofu Mokiwa amnbaye ni mdai, Mathew Kabunga kuwasilisha maombi ya kuondoa kesi.

“Baada ya kuwasiliana kwa kina na mteja wangu tunaomba kuondoa kesi chini ya kifungu namba 23 cha Sheria ya Madai, hayo ndio maelekezo ya mteja wangu,” alidai Wakili Mathew.

Wakili wa wadaiwa, Emmanuel Nkoma akijibu alidai hawana pingamizi sababu walioomba kuondoa kesi ndio walioleta kesim mahakamani lakini mahakama iangalie gharama ambazo wadaiwa waliingia tangu kesi hiyo ilipofunguliwa.

Hakimu Simba alikubali kuondoa kesi hiyo na kuwataka wadaiwa kupiga hesabu za gharama walizotumia kisha wawasilishe mahakamani.

Mwishoni mwa wiki Mokiwa aliwasilisha barua akiomba kuondoa kesi aliyofungua akipinga kustaafishwa kwa nguvu ili wakamalizane katika nyumba ya maaskofu.

Mokiwa aliiondoa kesi hiyo ya madai namba 20 ya mwaka huu aliyofungua dhidi ya Askofu Mkuu wa Makanisa ya Anglikana Tanzania Mhashamu Dk. Jacob Chimeledya na Bodi ya Wadhamini ya kanisa hilo.

Wakili wa wadaiwa, Gabrieli Masinga alidai walipokea barua kutoka kwa Wakili wa Askofu Mokiwa, Wakili Kabunga ikiwaelekeza waliwasilisha barua ya kuomba kuiondoa kesi mahakamani.

Alidai barua hiyo ilieleza sababu za kuondoa kesi hiyo ni kutokana na juhudi za kutatua mgogoro huo katika nyumba ya maaskofu.

“Wanaomba kuondoa kesi ili wapate muda wa kujadiliana kwani juhudi haziwezi kufanyika bila kesi hiyo kuondolewa mahakamani,”alidai.

Wakili Masinga alidai askofu huyo anataka kurejeshewa  uaskofu wake, anaomba mahakama itengue uamuzi wa kumstaafishwa kwa nguvu.

"Mokiwa aliondolewa Januari 7 mwaka huu akakimbilia mahakamani, mambo yanayohusu imani yanatakiwa kushughulikiwa katika nyumba za kiimani.

“Huwezi kuvuliwa madaraka msikitini ama kanisani ukakimbilia mahakamani, masuala hayo yanajadiliwa katika vyombo husika labda pakiwepo na ukiukwaji wa sheria za nchi,”alidai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles