22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

KESI NYINGINE YA KUPINGA SHERIA MPYA YA HABARI YAFUNGULIWA MWANZA

Karsan
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan

Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) na Kampuni ya Hali Halisi Publishers leo wamefungua kesi ya kikatiba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza wakidai ufafanuzi wa Mahakama juu ya sheria mpya ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 kukiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 18.

Mlalamikaji mkuu katika kesi hiyo ni UTPC akishirikiana na Hali Halisi Publishers ambapo tayari kesi hiyo imekwishafunguliwa na kupewa usajili namba 2/2017 ambapo jopo la wanasheria sita wataziwakilisha taasisi hizo katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanasheria Jenerali Ulimwengu kutetea maslahi ya umma katika kupata habari.

Akizungumza na wanahabari jana nje ya Mahakama Kuu, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan alisema baadhi ya vifungu vya sheria hiyo vinakandamiza uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza hivyo kukiuka Ibara ya 18 ya katiba ya nchi na kwamba kesi hiyo itasimamiwa na wanasheria Fulgence Massawe, Edwin Hans, Jenerali Ulimwengu, Jebra Kambole, Fransic Stolla na Mpale Mpoki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles