27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Kesi anayedaiwa kujaribu kumuua mkewe yapigwa kalenda

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

KESI ya kujaribu kuua inayomkabili mfanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Ombeni Mollel (33), imeahirishwa kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

Jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Chrisanta Chitanda, Jamhuri iliwakilishwa na Wakili Rose Sule.

Katika shauri hilo la jinai namba 19 la mwaka huu, Mollel anatuhumiwa kujaribu kumuua mke wake, Veronica Kidemi (30).

Jana kesi hiyo ilipangwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na wakili wa Jamhuri aliieleza mahakama upelelezi wake haujakamilika.

Hakimu Chrisanta aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2 itakapotajwa tena.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kujaribu kusababisha kifo kwa Veronica Septemba 25 mwaka huu katika eneo la Siwandeti, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Wakili huyo alidai mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai kifungu cha 211(a) kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles