23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kesi 1,519 zasikilizwa kwa mtandao ikiwa ni njia ya kujikinga na corona

Mwandishi wetu -Dar es Salaam

MAHAKAMA ya Tanzania imesikiliza mashauri 1,519 kupitia Mahakama Mtandao (Video Conferencing) kati ya Machi 23 hadi Aprili 21 mwaka huu, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, alilolitoa Machi 23.

Katika agizo lake akiitaka Mmahakama kutumia Tekknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) katika kupambana na virusi vya corona.

Mkurugenzi Msaidizi  wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Mahakama ya Tanzania, Machumu Essaba alisema mashauri hayo yamesikilizwa na mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Alisema Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilisikiliza na mashauri 424, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni mashauri 324, Mahaama ya Ilala mashauri 465 na Temeke 230.

Alisema mahabusu katika mashauri hayo, walisikiliza kesi zao wakiwa kwenye magereza ya Keko na Segerea.

 Katika hatua nyingine, Essaba alisema mahakama imeanza kutumia teknolojia maalumu inayomuwezesha jaji kusikiliza kesi akiwa ofisini bila ya kufika katika chumba cha mahakama ya wazi  au chenye vifaa vya  mahakama mtandao.

Alisema teknolojia hiyo imeanza kutumiwa na mahakama ya Tanzania  ikiwa ni njia mojawapo ya  kuepuka kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.

‘‘Teknolojia hii  inamwezesha jaji kusikiliza kesi  akiwa ofisini huku mhusika wa kesi akiwa katika chumba maalumu. Utaratibu huu hauruhusu watu wengine kuwa katika vyumba hivyo, isipokuwa wahusika wa kesi, ambao ni jaji na mleta maombi,’’alisema Essaba.

Mahakama imeanza kutumia teknolojia hiyo Aprili 21,  katika Mahakama ya Rufani Tanzania, ambapo Jaji wa Mahakama hiyo, Dk. Gerald Ndika alisikiliza kesi, akiwa ofisini kwake jijini Dar es salaam huku mleta maombi akiwa Mahakama Kuu Kanda Mwanza.

Uongozi wa mahakama katika  kuunga mkono juhudi za  Serikali kukabiliana na virusi vya corona tayari imekabidhi  vifaa vya Tehama  kwa maofisa wa kanda 16 za Mahakama Kuu  ili kuziwezesha kuanza kusikiliza  kesi kwa njia ya mahakama  mtandao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles