27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

KERI HILSON KUPAGAWISHA KENYA

NAIROBI, KENYA


MKALI wa muziki wa R& B nchini Marekani, Keri Hilson, ametua jijini Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kupagawisha kwenye tamasha la Terminal Music Weekend.

Msanii huyo alipokelewa na Mkurugenzi wa KICC, Mana Gecaga pamoja na nyota wa muziki nchini humo Habida.

Baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Nairobi, Keri alifanya mazungumzo na waandishi wa habari usiku wa manane na kudai hakutegemea kupewa mapokezi makubwa kama hayo.

“Ninajisikia furaha kuwa nchini Kenya, sikutarajia kupata mapokezi kama haya, ninawashukuru sana na ninatarajia kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wangu, hivyo wajitokeze kwa wingi,” alisema Keri.

Tamasha hilo la Terminal Music Weekend linatarajia kufanyika keshokutwa kwenye Ukumbi wa KICC, lakini kabla ya tamasha hilo msanii huyo atatembelea kwenye mfuko wake wa Keri Hilson Foundation uliopo Kibera, kilomita 6.6 kutoka jijini Nairobi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles