26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

KENYATTA AWAONYA WANAOBEZA MAKUBALIANO YAKE NA ODINGA

NAIROBI, KENYA


RAIS Uhuru Kenyatta amewakoromea viongozi wanaokejeli mpango wake wa kuungana na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga.

Bila kuwataja, Kenyatta alionya jaribio la kukwamisha mwafaka alioingia na Raila Machi 9, mwaka huu akisema halitafanikiwa.

“Baadhi ya watu wamekuwa wakiuliza, oh, kwanini umeenda kuzungumza na Raila? Yeye ni Mkenya na nina haki zote za kuzungumza naye, na wengine tayari kuwaunganisha Wakenya,” alisema Kenyatta katika viwanja vya Jacaranda mjini hapa juzi wakati alipotoa hatimiliki 50,000.

Aliongeza: “Namheshimu kila Mkenya, lakini sitotishwa na mtu yeyote. Msidhani kama mimi ni mtu wa kutishwa. Hapana!”

Katika taarifa ambayo inaonekana kuilenga kambi ya Naibu Rais William Ruto, Kenyatta alisema yuko tayari kuwapoteza washirika wake wa karibu ili abaki katika mwafaka na Odinga.

Baadhi ya viongozi wa Chama tawala cha Jubilee hasa wa kambi ya Ruto, wamekuwa wakihoji lengo la mwafaka aliofikia Kanyetta na Odinga.

Walimtuhumu Odinga kwa kutumia tukio hilo kuendesha kampeni ya kufanyika kura ya maoni kuhusu katiba na kujipanga urais mwaka 2022, madai ambayo ameyakana vikali.

Wakati Kenyatta akitetea mwafaka huo, Odinga alikuwa akikutana na mabalozi wa Umoja wa Ulaya (EU) katika makazi ya Balozi wa EU nchini Kenya, Stefano Dejak, akieleza makubaliano aliyofikia na Kenyatta.

Kauli ya Kenyatta kuwa hatishiki, ilichochewa na Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, alipomtaka kutotishika na uamuzi wake wa kumteua mwanaharakati wa upinzani, Miguna Miguna kuwa naibu wake gavana.

Katika shughuli hiyo ya ugawaji hatimiliki, Sonko alirudia mara kadhaa kuhusu watu waliopo Ikulu wanaomhujumu na kumtaka Kenyatta kutosikiliza maneno yao wanaposema hafanyi kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles