Kenyatta atengua uteuzi wa Waziri wa Fedha, amteua Waziri wa Kazi kushika nafasi yake

0
955
Waziri wa Fedha mteule wa Kenya, Ukur Yattan

Nairobi, KENYA

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametengua uteuzi wa Waziri wa Fedha Henry Rotich na kumteua Waziri wa Kazi, Ukur Yattan kushika nafasi yake.

Rais Kenyatta ametengua uteuzi huo leo Jumatano Julai 24, ikiwa ni siku moja tangu Rotich apandishwe kizimbani akikabiliwa na tuhuma za ufisadi kufuatia sakata la ujenzi wa mabwawa ya Kimwarer na Arror uliogharimu shilingi bilioni 19 za Kenya.

Rotich alikamatwa Julai 23, kufuatia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini humo, Noordin Haji, kutoa agizo la kumkamata pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Thugge Kamau na maafisa wengine wa Serikali kwa tuhuma za kufanya udanganyifu na kushindwa kutii muongozo wa unaotumika katika upatikanaji wa kandarasi.

Henry Rotich aliyekuwa Waziri wa Fedha kabla ya uteuzi wake kutenguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here