23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kenyatta ampongeza JPM kwa ushindi

Nairobi, Kenya

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemtumia salamu za pongezr  kwa Rais John Magufuli kwa kushinda uchaguzi uliofanyika Oktoba 28.

Rais Kenyatta alisema kuchaguliwa tena kwa Magufuli ni ishara ya upendo na imani waliyo nayo Watanzania kwa uongozi wake.

“Kwa niaba ya watu, Serikali ya Kenya na mimi mwenyewe nampongeza ndugu yangu, Dk John Pombe Magufuli kwa ushindi wako na wa Chama Cha Mapinduzi, katika uchaguzi uliomalizika..

 ”Nchi ya Kenya inatarajia kuendelea kufanya kazi na utawala wako kwa faida ya watu wa mataifa yetu mawili, kwa ustawi wa Afrika Mashariki na kwa amani, utulivu na ukuaji wa Bara la Afrika,”alisema.

Rais Kenyatta pia amemtakia Rais Magufuli afya njema na ufanisi anapojiandaa kuhudumu kwa muhula wa pili madarakani na kumhakikishia ushirikiano wa Kenya na kwa utawala wake .

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu.

Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa.

Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa.

Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles