24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Kenyatta, Akufo watoa somo kwa viongozi Afrika

Na BAKAR KIMWANGA – ALIYEKUWA NIGERIA


OKTOBA 25, mwaka huu Jiji la Lagos, nchini Nigeria lilifurika wajasiriamali vijana zaidi ya 5000 kutoka nchi za Afrika chini ya uratibu wa Taasisi ya Tony Elumelu.

Mkutano huo mkubwa unaokutanisha mataifa ya Afrika umefungua milango kwa wajasiriamali ambao ndiyo wameshika usukani katika kuimarisha uchumi wa nchi hizo.

Tanzania ni moja ya nchi za Afrika iliyokuwa na wawakilishi kwenye mkutano huo, huku ikitajwa ni moja ya nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi.

Tangu mwaka 2017 kasi ya ukuwaji uchumi wa Tanzania imefikia asilimia saba na moja ya chachu ya kasi hiyo inatajwa kuwa ni biashara ndogondogo ambazo kwa kiasi kikubwa zinamilikiwa na wanawake.

Kwa mujibu wa Takwimu za usawa wa kijinsia katika ajira zinaonesha kwamba kufikia mwaka 2014 Watanzania milioni 2.1 walikuwa wameajiriwa katika sekta rasmi, pamoja na serikalini na sekta binafsi, kwa mujibu wa kit- uo cha taifa cha takwimu nchini humo.

Hata hivyo takwimu rasmi za serikali zinaonesha pia kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wanawake walio kati ya umri wa miaka 18 hadi 24 yaani milioni 13.9 wanajishughulisha na shughuli zisizo rasmi yaani biashara ndogon- dogo na kilimo.

Hatua hii maana yake ni kwamba ni asilimia 0.75 tu ya wanawake walio katika umri wa kufanya kazi ndio wapo katika sekta rasmi.

Kwa maneno mengine, idadi kubwa ya wanawake walio katika umri wa kufanya kazi nchini Tanzania ni wajasiriamali.

Pamoja na kuwa na idadi kubwa ya wanawake wenye ujasiri wa kubuni na kuendesha biashara, kasi ya ukuaji wa mitaji yao bado ni finyu.

Chanzo kikuu cha mitaji karibuni duniani kote ni mikopo rasmi ya kibiashara. Hata hivyo, tafiti zinaonesha kuwa wanawake wengi wajasiriamali kutoka nchi zinazoinukia ikiwamo Tanzania hawana mikopo kutoka benki na taasisi rasmi za kifedha.

Utafiti uliochapishwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) mwaka 2014 unaonesha kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maombi ya mikopo ilitengwa kwa ajili ya wajasiriamali wanawake na asilimia 90 iliiva kwa ajili ya kutolewa.

Hata hivyo asilimia 18 ya wanawake wajasiriamali ambao waliomba mikopo benki na asilimia 28 waliomba mikopo katika taasisi nyenginezo za kifedha.

Jukwaa hilo la nne la kila mwaka liliwakutanisha wajasiriamali kutoka Afrika pamoja na viongozi wa sekta binafsi na umma walikusanyika jijini Lagos, Nigeria Alhamisi, Oktoba 25 mwaka huu la Taasisi ya Tony maarufu Tony Elumelu Foundation (TEF), Entrepreneurship Forum.

Tukio hilo ni fursa pekee ya kukusanya vipaji vya biashara kwa vijana, kujenga mitandao yenye nguvu na kupeleka ujumbe kwa watunga sera kwamba sekta binafsi iliyo mahiri inawajibika ina uwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Baada ya kupata mafunzo kabambe ya miezi tisa, ushauri na ufadhili, jumla ya vi- jana 4,470 walifaidika na programme hiyo iliyoshuhudia zaidi ya vijana laki tatu wakituma maombi.

Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, alisisitiza kuendelea kujitolea kuhakikisha maendeleo ya uchumi Afrika kwa kusaidia mafunzo ya kizazi kipya cha wajasiriamali ambao mafanikio yao yanaweza yakabadili bara hili ikiwamo kutengeneza ajira.

“Ujasiriamali ni muhimu kufungua maendeleo ya uchumi katika bara letu. Naamini kwa dhati mafanikio yanaweza yakaleta democrasia na kama tunaweza kubadili tamaa na kuwa fursa, hiki kizazi cha ajabu kinaweza kufanikiwa kwa kila jambo,” alisema Tony Elumelu

Kenyatta atoa somo Akihutubia mkutano huo kwa njia ya video kutoka nchini kwake, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliwaomba viongozi wengine wa Afrika kujenga mazingira bora zaidi kwa wajasiriamali wadogo ili kustawi kwa kutekeleza sera za kirafiki zaidi.

Aliwahimiza vijana kuwa na nguvu zaidi katika biashara na kupata taarifa zaidi ambazo zinaweza kuwawezesha kufanikiwa.

Rais Kenyatta alisema sekta za umma na za kibinafsi zinapaswa kuunga mkono juhudi

za Taasisi ya Tony Elumelu ili kuwawezesha vijana, ambao ni mgongo wa Afrika ili kutambua uwezo wao wa kiuchumi.

“Ni kazi yetu kukusaidia, si kupita njia yako. Ili kukusaidia vizuri, sisi sekta zote za umma na binafsi, tunahitaji kuja pamoja na kujunga mkono kazi ya Tony Elumelu Foundation,” alisema Rais Kenyatta

“Vijana, viongozi wa Kiafrika wenye ujuzi wanapigana kwa mabadiliko mazuri na kutumia teknolojia ili kuimarisha elimu na kutatua matatizo yaliyowasilishwa na huduma duni, ukosefu wa miundombinu na katika maeneo fulani katika bara, uharibifu wa kisiasa.

“Kweli, ukweli ni wazi; tunahitaji wanafunzi ambao wanaelewa ulimwengu wa kazi na tunahitaji mabadiliko ya suluhisho katika elimu ya juu au mafunzo ya ufundi. Safari ya elimu hadi kwenye kazi inahitaji kufanywa wazi na kazi iliyoandikwa kwa vijana katika vitu maalum katika safari,,” alisema

Alisema nchi imegeuka lango la maendeleo kwenye miundombinu ya ICT, kuhamasisha majukwaa ya simu ya kawaida ya kujenga mfumo mzuri, kuundwa

kwa maudhui ya ndani, kujenga uwezo wa rasilimali watu kunatokana na kutoa na- fasi za ajira kwa vijana ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka kila siku.

Wakati akitoa hutoba hiyo Ikulu ya Kenya, wajasiriamali wadogo 20 walihudhuria.

Rais aliwahimiza wajasiriamali wadogo kuona fursa zaidi na kutafuta ujuzi na kuzitumia kwa manufaa ya uchumi kupi- tia ajenda namba nne ya Malengo Endel- evu (SDG’s).

Rais Akufo-Addo Naye Rais wa Ghana, Nana Akufo- Addo, aliwasisitizia wawakilishi wa sekta ya umma kuhimiza, kusaidia na kuiga kazi inayofanywa na Taasisi ya Tony Elumelu.

“Hakuna kinachobadilika au kujiendeleza kivyake. Watu lazima waamke, waonge, wajadili na kubadilisha mada,” alisema Rais Nana Akufo-Addo.

Alisema wajariamali wadogo na wakati wamekuwa wakiendesha uchumi na nchi za Afrika hivyo wanahitaji kujengewa mazingira mazuri ya uwezeshaji.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, imeweza kuwasaidia wajasiriamali Waafrika kutoka pembe zote za bara hili na washindi katika mashindano mbalimbali katika jukwaa la mwaka huu walipata ufa- dhili wa dola za Marekani 5000 (takribani Sh milioni 11.4).

Na kwa mwaka huu wa 2018/2019 Taasisi ya Tony Elumelu imetangaza uwezeshaji kwa wajasiriamali wa Afrika zaidi ya Sh bilioni 22.9 kama njia ya kupambana na umaskini na soko la ajira kwa vijana kwa nchi za Afrika.

Wadau Kutokana na umuhimu wa jukwaa hilo la wajasiriamali wadau mbalimbali wame- unga mkono kazi hiyo chini ya Taasisi ya Tony Elumelu kupitia benki tanzu ya United Bank For Africa (UBA) ambayo inafanya kazi katika nchi karibu zote za Afrika.

Wengine ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na ICSRC.

Wajasiriamali wa Tanzania Baadhi ya wajasiriamali kutoka Tanzania, walieleza umuhimu wa jukwaa hilo la biashara kwani ni fursa ambayo inatakiwa kutumia na kila kijana.

Elia Kinshaga ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Kinshaga Food Products and Companies ni moja ya washiriki wa mkutano huo anasema moja ya bidhaa alizobuni ni biskuti zili- zotengezwa kwa ndizi ambazo zimekuwa na soko kubwa ndani na nje ya nchi.

“Nimekuwa nikitumia masoko ya ndani na nje lakini mimi kama mshiriki wa TEF 2018, nimefanikiwa kupata masoko kupitia teknolojia na jukwaa hili kwangu limekuwa na manu- faa. Ninaishuruku sana Tony Elumelu kwa ku- nipa fursa hii,” alisema Kinshaga

Carolyne Mahumba Mkurugenzi wa Kampuni ya Carvy Crafts Limited, aliwataka vijana nchini kuitumia mitandao ya kijamii kwa man- ufaa kwa kuangalia fursa mbalimbali duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles