23.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Kenyatta akemea ubaradhuli

NAIROBI, KENYA

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amefutilia mbali mpango wowote wa kujumuishwa suala la ubaradhuli kama moja ya ajenda za Kongamano la Kimataifa la Idadi ya Watu litakalofanyika wiki hii katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.

Rais Kenyatta alisema jana kuwa Kenya iko tayari kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa kimataifa kuhusu idadi ya watu lakini haitaruhusu vitendo ambavyo vinakiuka utamaduni wa Kiafrika.

Aliongeza kuwa; “Tutawakaribisha wageni Nairobi, na tutashiriki kongamano hilo na kusikiliza yatakayojadiliwa, lakini tutasimama imara kupinga kile ambacho hatukubaliani nacho.”

Mara kwa mara, Rais Kenyatta amekuwa akishikilia msimamo huo wa kupinga uozo huo, na jitihada za kujumuishwa uhusiano wa aina hiyo katika katiba ya Kenya.

Mei 24 mwaka huu, Mahakama Kuu ya Kenya ilifutilia mbali mpango wa kufuta au kuangalia upya sheria zinazoharamisha ubaradhuli nchini Kenya.

Nchi za Afrika zilizofuta adhabu kali kwa ubaradhuli ni Ushelisheli, Msumbiji, Sao Tome na Principe, na Lesotho

Haya yanajiri wakati huu ambapo Uganda inajiandaa kurejesha muswada bungeni ambao utatoa adhabu kali kwa mabaradhuli na wanaoendesha vitendo vichafu vya mahusiano ya watu wa jinsia moja, ikisisitiza kuwa vitendo hivyo vichafu vimeenea sana nchini humo na inabidi sheria kali ziwekwe ili kuvidhibiti.

Nchi za Afrika zimeharamisha na kupiga marufuku vitendo vya ubaradhuli na wanaopatikana na hatia ya kujihusisha na ufuska huo huandamwa na adhabu kali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,411FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles