KENYA YATANGAZA UCHAGUZI MPYA WA MCHUJO

0
386

NAIROBI, KENYA


RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ameomba radhi kwa kutojiandaa na mwitikio mkubwa wa wapiga kura uliolazimisha kufutwa kwa uchaguzi wa mchujo wa chama chake nchi nzima.

Kenyatta alisema chama cha Jubilee kitafanya uchaguzi mpya wa mchujo leo na kesho.

“Viongozi hawakutarajia mwitikio mkubwa wa watu kujitokeza kupiga kura na kusababisha upungufu wa karatasi za kura,” alisema.

Hilo lilisababisha vurugu kote nchini wakati wagombea walipowatuhumu wenzao kwa uchakachuaji.

Kenyatta alitarajia mwitikio wa asilimia 25 lakini uliotokea ulikuwa wa zaidi ya asilimia 70.

“Kura za mchujo kwa kawaida hazivuti mwitikio mkubwa wa wapiga kura kama tulioshuhudia Ijumaa iliyopita na hapo inaonesha hatukuwa tumejiandaa vyema," alisema.

Kati ya kaunti 21, ambazo kura za mchujo zilikuwa zifanyike, ni chache zilizoweza kuendesha.

Mchakato huo unafanyika kupata wagombea wa chama watakaochuana na wenzao pinzani wakati wa uchaguzi mkuu wa Agosti, ambapo pia rais mpya atachaguliwa.

Mwongo uliopita, watu zaidi ya 1,300 walikufa katika machafuko yaliyotokana na uchaguzi wenye utata, lakini wa karibuni uliofanyika mwaka 2013 ulikuwa wa amani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here