24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

KENYA YAPIGA MARUFUKU UINGIZAJI GESI KUTOKEA TANZANIA

Andrew Kamau

NAIROBI, KENYA

WIZARA ya Nishati nchini Kenya, imepiga marufuku uingizaji gesi ya kupikia kutoka Tanzania.

Uamuzi unatarajiwa kuibua uhaba wa nishati hiyo na kusababisha bei kupanda.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Andrew Kamau, mwanzoni mwa wiki hii, alisema wafanyabiashara hawataruhusiwa kuingiza gesi kupitia mipaka ya ardhini ndani ya wiki moja kuanzia siku hiyo.

Alisema kuwa hatua hiyo imelenga kuondoa mitambo haramu ya gesi za kupikia, ambayo imesambaa sehemu mbalimbali nchini humo na kuhatarisha usalama.

“Waziri ameandika barua kwenda Tume ya Usimamizi wa Nishati, Forodha na Shirika la Viwango Kenya, ikizitaarifu kuwa Mombasa ni kituo pekee cha kuingiza gesi ya kupikia.

“Iwapo unataka kushiriki biashara hii, njoo uwekeze Kenya, ingiza kupitia Mombasa, kisha hilo litatuwezesha kuwabaini wale wanaowasambazia wafanyabiashara wasio na vibali.

“Lakini sasa suala zima kuhusu Tanzania, ni suala lisilo na nafasi tena,” Kamau aliuambia mkutano wa Kampuni za Masoko ya Mafuta (OMCs), ulioandaliwa na Kampuni ya Mabomba ya Kenya.

Waziri Kamau, baadaye alithibitisha kwamba utekelezaji wa suala hilo utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu.

OMCs, zimekuwa zikilalamika kukwamishwa biashara zao na wafanyabiashara haramu wa gesi, ambao huchukua mitungi yao, kuijaza kisha kuirudisha sokoni.

Marufuku hiyo, inatarajia kuwaacha njia panda wafanyabiashara wa gesi inayotokea Tanzania, maana wengi wao wamekana kufahamu uwapo wa mpango huo.

Chama cha Wafanyabiashara wa Nishati, kilisema bado hakijapokea taarifa ya marufuku hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles