Kenya yang’ara mita 1,500 Olimpiki

Athletics - Women's 1500m Final

RIO DE JANEIRO, BRAZIL

KENYA imeng’ara tena kwenye michuano ya Olimpiki nchini Brazil, baada ya mwanariadha wao kwa upande wa wanawake, Faith Kipyegon, kushinda medali ya dhahabu.

Nyota huyo amefanikiwa kulitangaza taifa hilo kwa kuandikisha medali ya tatu ya dhahabu, huku akishinda mbio za mita 1,500 kwa wanawake.

Mwanzoni mwa wiki hii, mwanariadha kwa upande wa wanaume kutoka nchini Kenya, David Rudisha, aling’ara katika mbio za mita 800 na kutwaa medali ya dhahabu, hivyo kuifanya Kenya ifanye vizuri kwa Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Faith, amedai kwamba kwake ni furaha kubwa kung’ara kwenye mbio hizo za mita 1500 pamoja na kuiwakilisha Kenya.

“Nilikuja kwa ajili ya kushindana na kuipeperusha bendera ya taifa, nina furaha kubwa kuweza kufanya vizuri katika michuano hii mikubwa ya kimataifa, nilistahili kushinda dhahabu kutokana na maandalizi niliyoyafanya.

“Nawashukuru wote ambao walinipa moyo na waliniamini kuwa ninaweza kuiwakilisha vizuri nchi yetu, ninaamini dua zao zimenifanya nifanikiwe, hivyo ushindi huu ni kwa wale wote ambao walikuwa pamoja na mimi,” alisema Faith.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here