27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

KENYA YAIDHINISHA KUUNDWA BARAZA LA KISWAHILI

Nairobi, Kenya

Baraza la Mawaziri nchini Kenya limeidhinisha kuundwa kwa Baraza la Taifa la Kiswahili litakalokuwa na jukumu la kukuza na kuendeleza lugha hiyo nchini humo.

Pendekezo hilo linafuata kipengee 137 cha Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kinasema kwamba lugha ya Kiswahili itaimarishwa, kukuzwa na kutumika kama lugha ya Jumuiya hiyo.

Baraza hilo pia litatumika kutoa ushauri, kuimarisha miongozo ya serikali kuhusiana na kukuza, kulinda na kuunga mkono matumizi ya lugha ya Kiswahili.

Baadhi ya wahadhiri wa vyuo vikuu wamepongeza hatua hiyo akiwemo Prof Hezron Mogambi ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa sana.

“Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu kwa sababu maendeleo na ukuzwaji wa lugha ya Kiswahili yamekuwa yakikwama kwa sababu ya kukosa baraza kama hili. Matumizi sawa ya Kiswahili yamepigwa jeki,” amesema Mogambi.

Kwa muda mrefu, wasomi wa Kiswahili wamekuwa wakitegemea taasisi na vyama vya Kiswahili ambavyo sio vya serikali kukusanyika pamoja na kujadili masuala ya lugha ya kiswahili.

Miongoni mwa vyama hivyo ni Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA) kilichoanzishwa mwaka 1998 na Prof Kimani Njogu. Wasomi wa Kiswahili na wadau wengine wamekuwa wakihimiza kuundwa kwa baraza hilo kwa muda mrefu.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles