33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kenya kuwafunza watumishi wa umma DRC

NAIROBI, KENYA

KENYA imefungua ukurasa mpya wa uhusiano na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), baada ya kuahidi kuwapa mafunzo wafanyakazi wake wa umma katika harakati za kuiunga mkono serikali mpya ya Rais Felix Tshisekedi.

Tshisekedi anayazuru mataifa ya Afrika, wiki mbili tangu alipoapishwa kuiongoza nchi hiyo akianzia Kenya, ambayo Rais wake, Uhuru Kenyatta alikuwa pekee aliyehudhuria hafla ya kumuapisha Tshisekedi kati ya wakuu 17 wa nchi waliokaribishwa.

Kwenye kikao cha   Jumatano, akiwa kwenye Ikulu ya Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta alimuahidi Tshisekedi kuwa atawaunga mkono  kuleta ustawi wa  siasa katika nchi hiyo iliyotatizwa na vurugu wakati wa uchaguzi mkuu wa Desemba 30 mwaka jana.

Ili kufanikisha ahadi hiyo, wafanyakazi wa umma wa DRC watapewa mafunzo ya uongozi katika baadhi ya vyuo hapa kama vile Chuo cha Mafunzo ya Serikali cha Kenya.

Dhamira ni kutimiza ndoto za waasisi wa mataifa ya Afrika kwa manufaa ya ujirani mwema, aliweka bayana Rais Uhuru Kenyatta.

Kuhusu masuala ya biashara, viongozi wa mataifa hayo mawili wameahidi kuimarisha ushirikiano ikizingatiwa kuwa bidhaa nyingi za Congo zinapitia Bandari ya Mombasa zikielekea miji ya Goma na Lubumbashi iliyoko mashariki mwa Jamhuri hiyo.

Kwa upande wake, Rais Tshisekedi alimshukuru mwenyeji wake kwa kuwa rafiki wa dhati wa taifa lake hasa baada ya kuhudhuria hafla ya kumuapisha rasmi siku chache zilizopita.

Rais Tshisekedi kadhalika alikiri kuwa Bandari ya Mombasa ina mchango na umuhimu mkubwa na kuwa wako tayari kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuimarisha biashara ya kanda.

Viongozi hao wawili wameahidi kutembeleana Rais Tshisekedi atakapounda serikali yake mpya.

Mbali ya Kenya, Rais Tshisekedi ametembelea Angola na atamalizia ziara yake hiyo katika Jamhuri ya Congo jijini Brazzaville.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles