24.8 C
Dar es Salaam
Friday, October 4, 2024

Contact us: [email protected]

KENNA BLAKE: Dada anayetumia unene wake kujiingizia kipato

Joseph Hiza na Mitandao

MKAZI wa Boston, Massachusetts nchini Marekani mwenye uzito wa kilo 159, amekuwa akikumbana na kejeli kiasi cha kulazimika kuacha kwenda shule, sasa anaitumia fursa ya unene wake kujipatia fedha.

Kenna Blake alilazimika kuacha shule na kuamua kusomea nyumbani baada ya kuchoshwa na kebehi na matusi hivyo kumkosesha raha, sasa hutoza mashabiki wake kiasi cha fedha ili kumtazama akila akiwa mtupu. 

Kenna Blake (22), anasema aligeuka kuwa mtu wa kukejeliwa, mizaha, kebehi na kichekesho kutoka kwa watoto wenzake, huku wengine wakitengeneza video za kejeli kuhusu uzito wake.

Lakini sasa kejeli hizo zimegeuka kuwa kicheko na furaha kwake baada ya kupata mashabiki wanaovutiwa na uzito wake.

Kundi la mashabiki hao wanaopenda unene, humlipa kuanzia Sh 2,400 kwa wale wasio na fedha hadi 120,000 kwa dakika ili kumtazama pindi anapokula chakula akiwa na nguo ya ndani tu au mtupu.

Kenna aliona bandiko kuhusu mtandao wa ulaji na kunenepeana (feederism) – wakati akiperuzi blogu ya Tumblr miaka miwili iliyopita na kuamua kuanza kupost video zake mwenyewe.

“Nimejipatia mafanikio kwa kulipwa pindi ninapokuwa nikila pizza, kitu ambacho nina uhakika kwamba watu wengi hutamani kupata ajira kwa njia hiyo,” anasema na kuongeza:

“Maisha yangu yote ilinipasa kukabiliana na uonevu, kejeli, matusi na kila aina ya uchafu kuhusu uzito wangu. Shuleni mambo yakawa mabaya kiasi kwamba nikaamua kuacha shule nikiwa katika mwaka wangu wa kwanza tu, wakati nikiwa na umri wa miaka 14 nikaamua nisomee nyumbani.

“Kujiamini kwangu kulitatizika vibaya, lakini mtandao wa feederism ilirejesha hali yangu ya kujiamini. Nina furaha, hatimaye nimekutana na jamii ambayo inaukubali unene.

“Nilikejeliwa mara nyingi, wapo pia walionizomea wakisema sina thamani yoyote ile, lakini hapa unaweza kuona thamani yangu, watu wanatoa fedha ili kuniangalia nikila chakula.” 

Kenna, ambaye awali alijaribu bila mafanikio kuusaka wembamba baada ya unene wake kuwa kero, kwanza aliiona Tumblr baada ya kufanya kazi kwa muda kama msaidizi binafsi wa utunzaji watoto, mara baada ya kumaliza shule. 

“Sikuwahi kuisikia feederism kabla, lakini haikuchukua muda nilitambua kuna jamii inayojali mahali fulani.

“Kuanzisha ukurasa wangu mwenyewe ilikuwa kama kuanzisha blogu. Nilifuata taratibu na kufanya utafiti wangu,” anasema.

Tangu hapo, Kenna aliweza kujijengea ngome ya mashabiki wa kiume lakini pia wa kike, jamii ya watu wanaojivunia au kuvutiwa na unene.

Wakati alipoanza kwa mara ya kwanza, alijaribu kuongeza zaidi unene baada ya kubaini kuwa kuna jamii inayoupenda, akaona kuwa ni kazi ngumu kama lilivyokuwa jaribio lake lililoshindwa la kuwa mwembamba.

Hivyo, akaapa kuacha kudhibiti unene, badala yake kubakia na unene ule ule na mwenye furaha.

Kenna huwachaji watazamaji wake kuanzia Tsh 2,400 kwa dakika kwa video za kawaida; Sh 12,000 kwa dakika akila nusu mtupu, au Sh 24,000  kwa dakika akiwa mtupu hadi Sh 120,000.

Hata hivyo, aligoma kufichua kiasi gani anatengeneza kwa video zake hizo kwa wiki.  

Anasema: “napost video moja kwa wiki, wakati watazamaji wakipata fursa ya kuihariri vizuri. Hujaribu kuzifanya ziwe angalau za urefu wa dakika nne, lakini wakati mwingine napost fupi zaidi ambazo ni za bei rahisi.

“Hizi ni kwa wale wanaopenda kuniunga mkono, lakini bahati mbaya hawana fedha za kutosha.”

Mbali ya picha na video anazotupia mtandaoni kwa ajili ya mashabiki wake, Kenna hutuma mara kwa mara ujumbe kuhusu maisha yake ya kila siku, ili kujenga ukaribu na uhusiano na mashabiki wake.

Anaongeza: “Hufanya kile ninachokiita ‘mazungumzo ya unene’, ambapo watu huweza kuniangalia nikizungumza namna inavyokuwa ukiwa mnene na namna jamii inavyoitikia.

“Sitaki kuishia katika biashara tu maana nina mashabiki wanene katika ukurasa wangu, waliopitia mateso kama mimi au kunizidi na hivyo ninachofanya ni kuwasaidia wajisikie vizuri kwa vile hawako peke yao.”

Pamoja na mabadiliko hayo Kenna bado anakabiliwa na kejeli, hujikuta akipata mashambulizi mitandaoni.

Kwa mfano, katika mtandao wa Instagram, watu huzichukua picha zake na kuzisambaza kwa marafiki zao ili kumgeuza kituko.

Hata hivyo, kwa sasa nimekomaa na ninachofanya ni kuwafungia mawasiliano.

Anasema amewasamehe wale wa utotoni waliomkebedhi akisema baada ya kukua anaamini watakuwa wametambua makosa yao kwamba kila mtu anastahili heshima.

Kwa sasa amepanga kupanua zaidi kundi la mashabiki wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles