26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

SWAGGAZ, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma zake kama No Dulling, Aluguntugui, Sorkode, Today, Same Girl, Diabetes na nyingine kibao zilizowatambulisha vyema ndani na nje ya nchi hiyo.

Kundi hilo ambalo linaundwa na wasanii wawili ambao ni Joshua Ampah na Andrew Cudjoe huku lengo lao likiwa ni kuwafikia mamilioni ya mashabiki wanaopatikana Afrika Mashariki (East Africa).

Swaggaz: Kwa ambao bado hawaja wafahamu, Keche ni kina nani?

Adrew Cudjoe: Keche ni kundi la muziki wa kizazi kipya kinachofanya muziki wa Afro Pop au Hiplife kutoka hapa Ghana kilichoanzishwa zaidi ya miaka kumi iliyopita na tunajulikana zaidi hapa kwetu kwa ngoma zetu zilizofanya vizuri.

Swaggaz: Kwanini mliamua kujiita Keche?

Joshua Ampah: Keche inamaanisha ‘skills’ yaani ujuzi kwa lugha ya Akan ya hapa Ghana na hiyo imekuwa ikiakisi kazi tunazofanya kwa sababu ngoma zetu zote huwa zina ubunifu na ujuzi wa hali ya juu.

Swaggaz: Changamoto zipi mnakutana nazo kwenye muziki wenu Ghana?

Adrew Cudjoe: Changamoto zilikuwepo mwanzoni wakati tunaanza ila kwa sasa tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Keche ni miongoni mwa makundi makubwa hapa Ghana na sasa tunaitazama zaidi ‘game’ la ‘east Africa’.

Swaggaz: Lini mlitambua muna kipaji na mnaweza kufanya kazi pamoja?

Joshua Ampah: Mwanzoni mwa mwaka 2000 mimi nilianza kwa kupenda kucheza mpira wa kikapu na mpira wa miguu kwenye shule ya sekondari ya St John Senior. Hapo ndio nilikutana na mwenzangu Andrew ambaye alikuwa mwanafunzi na yeye alikuwa anapenda sana riadha.

Ila tofauti ni kwamba mimi natokea Mkoa ambao upo katikati ya Ghana na Andrew anatokea Mkoa ambao upo Magharibi ila wote wawili tuna uwezo mkubwa wa kuimba na kufanya ‘freestyle’.

Kufikia mwaka 2005, tulikuwa tumeanza kurekodi demo na ‘mixtapes’ nyingi kama One Blaze na Dons Mic zote tulifanya kwenye studio za Tema Metropolis tukapata nafasi kurekodi kwenye studio za Highly Spiritual chini ya prodyuza maarufu Kaywa.

Mwaka 2008 kundi letu la Keche lilianza kupata umaarufu kupitia wimbo wetu, Omogemi na ikafuatiwa na kolabo yetu tuliyofanya na Sarkodie inayoitwa Ring Well Bell iliyotuchongea njia ya mafanikio.

Swaggaz: Mna mipango gani kwa sasa na wasanii gani wa Tanzania mnatamani kufanya nao kolabo?

Andrew Cudjoe: Kwa sasa tunaliangalia zaidi soko la Afriuka Mashariki na Tanzania ndio kitovu cha muziki. Tuna mpango wa kujana Bongo na kwa sasa tunafikiria kufanya kolabo na Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Lavalva na wengine.

Kwa sasa tumetoa video ya wimbo wetu No Dulling ambao tumemshirikisha Kuami Eugene ambao mpaka sasa umetazamwa na watu wzaidi ya milioni 1.8 kwenye chaneli yetu ya YouTube ya GEM MEDIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles