23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

Kebwe azindua Maghala sita ya nafaka

Mwandishi Wetu – Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe amezindua maghala sita ya kuhifadhia nafaka ambayo yamejengwa au kukarabatiwa na Mradi wa Kupunguza upotevu wa Mpunga wakati na baada ya mavuno (RIPOMA),

 Maghala hayo ambayo yamejengwa katika wilaya za Kilosa na Mvomero na yanatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya wananchi 15,000 kaya 3005 kwa kupitia vikundi 101 vya wakulima wanawake na vijana katika vijiji 36.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo Septemba 12, mwaka huu wilayani Kilosa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Steven Kebwe alisema maghala hayo  yatakuwa vituo vya kukusanyia nafaka kwa ajili ya kuuza kwa pamoja ili kupata bei nzuri na njia rahisi ya kupata mikopo kupitia benki.

Naye Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya Anna Costantine alisema EU kwa kushirikiana na HELVETAS,  wamejipanga kukuza  sekta ya mpunga  katika mkoa  wa Morogoro.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi wa HELVETAS, Daniel Kalimbiya Maghala haya yamegharimu Sh Milioni 508.56 (EUR 200,000), ikiwa ni mradi wa Kuwawezesha Wakulima wadogo (Wanawake na Vijana) kupitia mradi huo.

“Maghala haya yamegharimu Sh508.56 hii ilikuwa ni moja ya mradi wa Kuwawezesha Wakulima wadogo (Wanawake na Vijana) kupunguza upotevu wa Mpunga wakati na baada ya mavuno.

RIPOMA ni mradi wa miaka mitatu (Julai 2017 mpaka Juni 2020 wenye bajeti ya EUR 1,875,000 (Sh Bilioni 4.768) ambapo Umoja wa Ulaya (EU) umechangia 80% na HELVETAS 20%.

HELVETAS inatekeleza mradi huu kwa kushirikiana na Community Development and Relief Trust (CODERT), Small Industries Development Organisation (SIDO), JRT Agri-services (JRT), DBB Agro-Initiative, Halimashauri za Wilaya na Serikali ya Tanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles