29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

KCU Kagera chatoa bilioni 1.4 kwa wakulima wa kahawa

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kagera (KCU 1990 Ltd) kinachojihusisha na kukusanya Kahawa kutoka kwenye vyama vya msingi ambavyo ni wanachma wa KCU katika baadhi ya wilaya mkoani humo kimetoa zaidi ya Sh bilioni 1 .4 kwa wakulima wa zao hilo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Ressy Mashulano wakati akizunguza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa ofisi ya chama hicho zilizopo katika Manispaa ya Bukoba.

Hata hivyo, amesema kuwa kama yalivyo majukumu ya chama hicho kuhakikisha wakulima wa zao la kahawa mkoani Kagera wananufaika zaidi, chama hicho kimetoa fedha hizo kama nyongeza ya malipo ya zao hilo kwa msimu wa 2021/2022.

“Wakati tunaelekea kwenye msimu mwingine, chama kikuu cha ushirika mkoa wa Kagera kimeweza kutoa kiasi cha Sh bilioni 1.4 na hii nikutokana na kile tunachokipata ndo hicho tunakirudisha kwa wananchi,” amesema Mashulano.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Respicus John amesema kuwa, chama kikuu cha ushirika mkoani Kagera (KCU 1990 Ltd) kupitia kwa viongozi wake wamepanga mikakati mbalimbali ili kuhakikisha chama hicho kinatimiza matarajio ya wakulima hao wa kahawa.

“Tumepanga mpango mkakati kwa miaka mitano ambao umesheheni mambo mbalimbali, tuna mradi mkakati ambayo tumejipanga kuifanya kama vile mradi wa kilimo cha kahawa katika mashamba yetu ya chama ambayo yatatumika kama shamba darasa hapa mkoani Kagera.

“Pia kuanzisha ujenzi wa miradi ya vitega uchumi kwani mnajua kuwa chama chetu kimewekeza katika majengo na tunayo ardhi tupu inayohitaji kuendelezwa pamoja na majengo ambayo hayajafikia kiwango , hivyo kupitia wadau mbalimbali tutahakikisha tunayaendeleza na tunaamini kuwa endapo miradi hii ikitekelezwa itaweza kubadili sura ya mji wetu wa Bukoba na kuongeza mapato ya ndani ya chama,” amesema John.

Ameongeza kuwa, chama hicho kimejipanga kuanzisha mfuko maalumu ambao utawawezesha wakulima wa kahawa kuweza kukopeshwa fedha ili kuweza kukidhi mahitaji yao kwani wakulima wengi vijijini wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya kukoswa mikopo suala ambalo limepelekea wananchi hao kipindi amchacho sio cha msimu kuuza kahawa zao kwa njia za ‘obutula’.

“Kupitia mfuko huu maalumu kama mambo yataenda vizuri wakulima watakuwa wanakopa fedha kipindi ambacho sio cha msimu na wakati wa msimu unapofika basi wanaleta mazao yao kwaajiri ya kulipa mkopo huo “ amesema John.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles