24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, October 24, 2021

KCB 2JIAJIRI YALETA MAFANIKIO NCHINI

NA HARRIETH MANDARI-DAR ES SALAAM


BENKI ya KCB Tanzania iliendesha programu ya KCB 2jiajiri Malkia wa Nguvu jijini Dar es Salaam kwa wajasiriamali ambao ni wanachama wa huduma mpya ijulikananyo kama ‘ KCB 2jiajiri pamoja na wasiowanachama’.

Tamasha lake lilifanyika katika ukumbi wa King Solomon na kuhudhuriwa na wanawake wajasiriamali zaidi ya 1,500 ambao walisherehekea, kuonesha bidhaa zao na kuunda mitandao ya kibiashara ili kukuza masoko yao.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Dr. Ashatu Kijaji, na Waziri wa Biashara na Viwanda  Zanzibar, Amina Salim Ally, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Bi. Zuhura Sinare Muro na wajumbe wengine wa bodi ya KCB.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Dk Ashatu alisema ili wanawake wa Tanzania waweze kuchangia pato la taifa, ni lazima kwanza kuwa wabunifu na wenye nia thabiti ya kufanya biashara.

“Kuna mwanamke mmoja alikuja pale ofisini kwangu akiwa na wazo zuri tu la kuanzisha kituo cha kulea watoto wakati wa saa  za kazi ambapo wazazi wengi wasio na wasaidizi majumbani mwao wamekuwa wakihangaika jinsi ya kuwalea watoto hao katika mikono salama, lakini nilipomuuliza nia yake kubwa ya kuchagua biashara hiyo akasema ni kupata pesa nilimkatalia kwa kuwa alitanguliza mbele pesa hivyo kuweka shaka katika utekelezaji wake kwa uaminifu, na nilimkatalia kumpa msaada wa mtaji,”alisema.

Akaongeza kuwa watanzania wengi bado wana haraka ya kupata pesa kwa njia ya mkato hali ambayo ni hatari katika sekta ya biashara.

Akizungumza katika tukio hilo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Masika Mukule alisema kwamba kongamamno kama hilo linaloandaliwa na Benki hiyo chini ya ‘KCB 2jiajiri’ ni endelelvu, ambapo benki hiyo   itawezesha wanawake wajasiriamali (women empowerment/capacity building) ambayo ilizinduliwa rasmi Desemba, 2016, na hadi  sasa wamewezeshwa  stadi za biashara endelevu wanawake 258 kutoka mikoa sita , ambayo ni Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Morogoro na Zanzibar.

“KCB 2JIAJIRI” ina lenga kuondoa vikwazo  vinavyowakwamisha wanawake  kama vile haki ya kumilikimali,  kuanzisha ajira na sheria na kanuni  ambazo zimewakwamisha wanawake  dhidi ya manufaa, biashara endelevu na maisha yaliyoboreshwa. Mradi huo unatekelezwa kwa ushirikiano na Kituo cha Ushindani na Ujasiriamali Tanzania (TECC) ambapo inawezesha wanawake wanaoshiriki kujitegemea, kuwa huru kiuchumi na kudhibiti ustawi wao kiuchumi na kijamii,” alifafanua Mukule.

Akaongeza kuwa mradi huo upo katika sera ya benki hiyo ya uwekezaji kijamii ambayo inatoa kipaumbele kujihusisha kijamii zaidi, ambapo  lengo lake kuu ni kunyanyua maisha ya jamii.

Akabainisha kuwa Benki ya KCB  inatambua mchango mkubwa wa wanawake wanaoutoa katika sekta binafsi hususani katika Ujasiriamali mdogo na wakati (SMEs) na kuongeza kuwa  shughuli zao zina kumbana na  changamoto nyingi pamoja na upatikanaji wa mtaji, ufahamu finyu wa mambo ya kifedha, Utunzaji wa kumbukumbu za kifedha, Kufikiwa na huduma za kifedha, Sera ongozi za biashara na upatikanaji wa masoko.

“Hivyo Lengo letu kwa ujumla ni kuwezesha wafanyabiashara wanawake wa Kitanzania kuandaa mikakati ambayo inaboresha stadi zao na uwezo hivyo kuunda fursa nyingi za kibiashara kwa ajili yao.”Aliongeza.

Mmoja wa wanufaika wa mikopo kutoka benki hiyo ambaye alishiriki kongamamno hilo, Rukia Chambega alisema amekuwa akinufaika na situ mikopo bali mafunzo ya jinsi ya kutunza fedha, kutafuta masoko na pia jinsi ya kutunza kumbukumbu katika biashara.

“Tangu nipatiwe mafunzo hayo nimeweza kutunza vizuri kumbukumbu za biashara yangu niliyoanza nayo ya duka la nguo na nikafanikiwa kufungua saluni ya wanawake,”alisema.

Wale wanaofanikiwa kuhitimu Programu ya KCB 2JIAJIRI wanapata fursa ya kipekee ya kujiunga na Klabu ya Biashara ya KCB ambayo inawaunganisha na jumuia za kibiashara za kitaifa na kimataifa. Kadhalika wananufaika hupata huduma ya washauri watatu katika nyanja za Kifedha, Kisheria na Masoko kwa kuwapatia ushauri wa kibiashara na kitaalamu.

Benki ya KCB ni benki   iliyoanzishwa mwaka 1896 kisiwani Zanzibar. Benki hiyo  imekua na kuenea katika nchi za Tanzania, Kenya Sudani ya Kusini, Uganda, Rwanda, Burundi na Ethiopia.

Hadi sasa, Benki  ina mtandao mkubwa zaidi katika kanda hii ikiwa na matawi 250, mashine za kutolea fedha (ATM) 962, na wakala 12,000 wanaotoa huduma za benki masaa 24 siku saba za wiki katika Afrika Mashariki. Benki ya KCB imesajiliwa katika soko la hisa la Nairobi, Dar es Salaam, Uganda na Rwanda. KCB Bank Group pia linamiliki kampuni ya bima ya KCB, KCB Capital na KCB Foundation.

Nchini Tanzania, KCB ilifungua milango yake mwaka 1997 na toka hapo imekuwa mdau mkubwa katika kukuza sekta ya fedha nchini. Kwa sasa benki ina matawi yapatayo 14 Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar. 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,967FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles