Na WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
WAKATI leo ukiwa ni mwanzo wa matumizi mbadala wa mifuko ya plastiki kama ambavyo sheria na kanuni za Usimamizi wa Mazingira za kupiga marufuku mifuko hiyo za mwaka 2019 zinavyoelekeza, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) tayari jana lilianza kazi ya kusambaza maofisa wake kwa ajili ya kukagua utekelezaji huo.
Akizungumza jana Mwanasheria wa NEMC, Manchare Heche alisema maafisa hao ambao wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo viwandani na katika maduka makubwa wamefanya kazi ya kukagua na tayari wamekuta kiwanda kimoja kikiwa na tani 100 za mifuko hiyo.
“Nasubiri maafisa ambao walikuwa katika maeneo mbalimbali nchini kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo ili niweze kutoa takwimu sahihi za shehena za mifuko ya plastiki zilizosalimishwa,” alisema Heche.
Alisema mwitikio wa watu katika zoezi hilo ni mkubwa na hasa katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
“Mwitikio ni mzuri mfano Mkuranga viwanda vyote vimeshafungwa na kusitisha uzalishaji,kuna kiwanda tumekikuta na zaidi ya tani 100 na wameshafunga,”alisema Heche.
Kupitia ukurasa wake Twitter, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, Janaury Makamba aliandika kuwa …
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA