MSHINDI wa shindano la Bongo Star Search (BSS) 2015, Ismail Juma ‘Kayumba’, amedai licha ya kufanikiwa katika muziki hatasahau aliposingiziwa wizi alipokuwa akifanya biashara ya madera na viatu Manzese jijini Dar es Salaam.
Kayumba alieleza hayo juzi alipotembelea Ofisi za New Habari (2006) Ltd inayochapisha magazeti ya Mtanzania, Bingwa, Dimba, Rai na The African.
“Mwajiri wangu aliniachia niuze madera aliporudi jioni akaangalia hesabu akasema kuwa nimeiba fedha kutokana na hesabu kwenda tofauti na alivyotaka akanipeleka kituo cha polisi.”
“Baadaye polisi walifuatilia hesabu vizuri ikagundulika sikuchukua fedha yoyote wakaniachia huru, kitendo hicho kiliniumiza sana ndicho kilichonisababisha niachane na biashara na kuingia katika muziki ambao naendelea kuufanya kwa mafanikio,” alisema.