25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kayumba kufuta makosa katika video mpya  

KayumbaNA FESTO POLEA

ANAYESHIKILIA taji la ushindi la Bongo Star Search (BSS) 2015, Juma Kayumba, ambaye anatamba na wimbo wa ‘Katoto’ amesema hatarudia makosa aliyofanya katika wimbo wake wa Kitoto.

Kayumba aliliambia MTANZANIA kwamba yupo mbioni kufanya video ya wimbo wake mpya wa ‘Dengua’ ambao bado haujaachiwa popote akiamini kwamba amejifunza mengi katika video yake ya kwanza.

“Nimejifunza kitu katika video ya ‘Katoto’ maana sikuwa nikijua kinachoendelea nililetewa mwanamke mkubwa ingawa alicheza vizuri katika video yangu lakini hatukulingana yeye ni mkubwa sana kwangu hivyo katika video hii mpya nitatafuta msichana tunayelingana ili aendane vyema na hadithi ya wimbo wenyewe.

“Wimbo ni wa mapenzi unataka kuwe na msichana atakayekuwa akiringa na kudengua, bado sijajua kama nitasafiri kwenda Afrika Kusini au nitapiga picha zake hapa hapa Dar,” alisema Kayumba akidai ataanza harakati hizo mwishoni mwa mfungo wa Ramadhani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles