24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KAYA MILIONI MOJA ZAANDIKISHWA TASAF

Ramadhan Hassan, Dodoma


Serikali imesema kaya maskini milioni 1.1 zenye jumla ya watu milioni tano zimeandikishwa katika Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini (TASAF) katika vijiji 9,986.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa Septemba 7,  alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha (Chadema) ambaye katika swali lake Msabaha alihoji ni kwa kiasi gani mradi wa kusaidia kaya masikini (TASAF) umeweza kuwasaidia Wananchi hususani katika Visiwa vya Pemba na Unguja.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuchika amesema mpango wa kunusuru Kaya maskini ulianza rasmi Januari 2013 ambapo mpango huo ni wa miaka 10 iliyogawanyika katika vikundi vya miaka mitano na unatekelezwa hadi mwaka 2023 katika Halmashauri zote Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema kwa upande wa Zanzibar Kaya zilizonufaika na Mpango huo kwa kupatiwa ruzuku na ajira kwa kushirikii katika kazi ili kutoa ajira.

Waziri Mkuchika alisema jumla ya shilingi bilioni 32,698,501.00 zimetumika toka mpango huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles