31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Kaya masikini katika vijiji 43 Arusha DC kunufaika na Mpango wa Tasaf

Na Mwandishi Wetu, Arusha
KAYA masikini kutoka vijiji 43 vya

Halmashauri ya Wilaya ya Arusha mkoani Arusha zinatarajiwa kunufaika na mamilioni ya Mpango wa Kunusuru Kaya maskini (TASAF) awamu ya tatu.

Hayo yamebanishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Seleman Msumi, wakati akizungumza katika kikao kazi kilichoshirikisha wawezeshaji watakaokwenda kubaini kaya maskini ambazo zitaingia katika kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya TASAF.

Amesema maisha ya walengwa wa mradi huo yanakwenda kubadilika.

Mkurugenzi huyo amesema wawezeshaji hao wameaminiwa na serikali katika kutekeleza majukumu hayo hivyo wanapaswa kuzingatia uadilifu ili mpango huo uweze kuleta tija kwa kuwanufaisha walengwa na kuwaondoa katika lindi la umasikini ili waweze kujiinua kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

“Wale ambao mmeaminiwa kusimamia zoezi hili, mpango huu unatakiwa uwafikie walengwa kwani kumekuwa na baadhi ya malalamiko kutoka awamu zilizopita kuwa fedha zilienda kwa watu ambao siyo walengwa,” amesema Msumi.

Naye Meneja wa miradi ya ajira za muda kwa kaya za walengwa TASAF Makao Makuu, Paul Kijazi, amesema katika awamu iliyopita walifikia kaya milioni 1.01 ambazo ni sawa na zaidi ya watu milioni tano na kuwa awamu ya sasa unatarajia kufikia kaya na vijiji vyote Tanzania Bara na Zanzibar, ambavyo havikuweza kufikiwa katika awamu zilizopita.

Amesema kikao kazi hicho ni muhimu na kuwa wameshapita katika kanda tatu kwa ajili ya kupata vijiji ambavyo havikuwa katika mpango huo wa tatu kipindi cha kwanza na kuwa vijiji asilimia 30 nchi nzima havikuwa vimenufaika na mpango huo hivyo kufikiwa awamu hii.

Alisema katika awamu hii wamepata Dola milioni 800 ambazo ni zaidi ya Sh trilioni 2 kutoka Benki ya Dunia huku Serikali ikitarajia kuchangia Sh bilioni 15 kwa ajili ya mchakato huu na kuwa bado wanaendelea kutafuta wafadhili wengine.

Mratibu wa Tasaf halmashauri ya Arusha, Grace Makema,alisema katika awamu hii wanatarajia kufikia vijiji 43 ambavyo vilibaki na kuwa katika awamu ya kwanza waliweza kufikia vijiji 45.

“Matarajio yetu ni kuhakikisha tunafikia walengwa wenye uhitaji kwa sababu huu mpango unashirikisha kuanzia ngazi ya jamii kule chini kabisa kijiji na wananchi wenyewe ndiyo wenye mamlaka kusema nani anastahili kuingia katika mpango,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles