33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kawasso wataka uhalali vitambulisho vya machinga

Christina Gauluhanga Na Tunu Nassor, Dar es salaam

UMOJA wa Wafanyabiasha Wamachinga wa Kariakoo (Kawasso), umeiomba Serikali kuunda chombo maalumu cha kuthibitisha uhalali wa vitambulisho wanavyopewa Wamachinga ili kuondoa sintofahamu iliyopo hivi sasa kwa wafanyabiashara wakubwa kumiliki vitambulisho hivyo.

Akizungumza na MTANZANIA jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kawasso, Namoto Namoto alisema uwepo wa kikosi kazi maalumu utasaidia kuondoa ujanja unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa na kuchangia kupoteza Mapato stahili ya Serikali.

Alisema kutokuwapo kwa ufuatiliaji wa vitambulisho hivyo kutasababisha mwaka ujao wa fedha watu wengi kukosa Imani ya kuchukua vitambulisho hivyo tena.

“Nashauri kuwapo kwa kikosi kazi cha kukagua vitambulisho vya Machinga kwani kwa sasa aliyenacho na asiyenacho wote wanafanyabiashara pia Kuna tuhuma kuwa hata wafanyabiashara wakubwa wamejipenyeza humo jambo linalowafanya waliovichukua wasione umuhimu wake,”alisema Namoto.

Aliwaomba wateule wa Rais Dk.John Magufuli kusimamia vema maelekezo na kiongozi ya rais kuhusu wafanyabiashara wamachinga na kutenda haki kwa wote.

Alisema haina maana endapo kuna baadhi ya wafanyabiashara hadi leo wanaendelea kujipenyeza kwa kuuza biashara zao huku wakiwa hawana vitambulisho.

Namoto alisema viongozi wa Wamachinga ni sehemu husika washirikishwe wakati wa ugawaji vitambulisho hivyo ili kufahamu uhalali wa kila mtu anayepewa umiliki wa vitambulisho hivyo.

Aliongeza kuwa katika uundwaji kamati hizo viongozi Wamachinga wakashirikishwa katika kamati za ukaguzi wa vitambulisho wakihusishwa maofisa biashara, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na Mamlaka zingine ili kubaini wanaovimiliki na wasio navyo ikiwa ni pamoja na utoaji adhabu kali kwa wasio na vitambulisho kwa kuwa hawachangii huduma za Serikali.

Namoto alisema Wamachinga pia wanaomba Mamlaka ya Maji Safi na Taka (DAWASA), kuwaondolea changamoto za maji taka kwenye baadhi yya Mitaa teule ya kufanyia biashara zao kwakuwa imekuwa ni changamoto kwao.

Alisema Kuna baadhi ya mitaa kimekuwa na miundombinu ya majitaka ambayo ni mibovu imekuwa ikitiririsha maji taka kila kukicha na kusababisha hatari ya magonjwa ya mlipuko na kusimamia kwa biashara kwa siku mbili hadi tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles