26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

KAULI ZA SUMAYE, LOWASSA IKULU ZAIBUA MJADALA

Na MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM


KAULI zilizotolewa juzi Ikulu, Dar es Salaam na Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya tatu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa, aliyeshika wadhifa huo wakati wa awamu ya nne, zimeibua mjadala miongoni mwa wanajamii.

Baadhi ya watu wameonyesha kutomwelewa Sumaye, hasa katika kauli aliyosema “nina hakika kwenda kwangu huko kutakuwa pia ni kwa faida kwa CCM”.

Wengine wameonekana kubishana kwenye kauli ya Lowassa, aliyomnukuu Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere, juu ya kipimo cha nchi yenye amani. Baadhi walimpongeza na wengine wakisema maneno yake hayajaeleweka.

Kutokana na kauli za wastaafu hao, baadhi ya wachambuzi waliongea na gazeti hili jana waliwatetea na wengine kuwakosoa.

PROFESA BAREGU

Akizungumzia kauli hiyo, mchambuzi wa masuala ya siasa, Profesa Mwesigwa Baregu, alisema Sumaye aliona CCM ni chama cha siasa kilichoishiwa pumzi, hivyo akaona akaweke nguvu upande wa pili.

“CCM haiwezi kuwepo bila kuwepo upinzani imara na ujenzi wa demokrasia imara katika nchi yetu, na baada ya upinzani kuimarika itakuwa kwa faida ya masilahi ya taifa, ndivyo nilivyomwelewa,” alisema Profesa Baregu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Kwa habari kamili jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA hapo juu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles