27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

KAULI YA JPM YAMSHANGAZA LOWASSA

Na Mwandishi Wetu-PWANI


WAZIRI Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amemwomba Rais Dk. John Magufuli kufuta kauli yake ya kuwazuia wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),  kushirikiana na wabunge wa upinzani.

Akizungumza jana katika ziara viongozi wa Chadema katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam, Lowassa alisema kauli hiyo Rais Dk. Magufuli inabomoa misingi ya amani iliyojengwa na waasisi wa taifa letu.

'”Namuomba Rais (Magufuli)  aondoe kauli ile aisahihishekauli hiyo na nawaomba watanzaniatukatae kugawanywa…tusikubali nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa ikienda vibaya tunaangamia wote ikienda vizuri tunafaidi wote kwahiyo tukatae,” alisema

Alisema Watanzania wamekuwa wakiishi bila ya kubaguana kwa misingi ya dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka kuiacha.

Mjumbe wa huyo wa Kamati Kuu alisema hali ya maisha imezidi kuwa ngumu, huku bei ya bidhaa ikizidi kupanda kila siku.

Kutokana na hali hiyo alisema CCM kiliiba sera ya Chadema, ikiwemo elimu bure, lakini imeshindwa kuitekeleza.

“'waliiba sera na ilani yetu ya uchaguzi, lakini kwa kuwa hawakujiandaa wamefanya hali kuwa ngumu sana,” alisema

Katika kikao hicho cha ndani cha kuimarisha chama, Lowassa ameeleza tatizo la ajira linavyozidi kuwa kubwa na kuongeza kuwa mipango mibovu imesababisha sekta binafsi kuyumba, huku makampuni kadhaa na shughuili nyingine za kutoa ajira zikifungwa na kusababisha ongezeko kubwa la wasiyo na ajira.

Kuhusu ushirikiano miongoni mwa vyama vya upinzani, Lowassa alisema Ukawa ni muhimu kuliko wanavyoweza kudhani kwani muunganiko wa vyama vya siasa katika karne hii ni jambo la muhimu.

“Kikubwa cha kuzingatia ni umoja na mshikamano. Watanzania wana imani kubwa sana na chadema kwa sasa na kama kuna mtu anatafuta chama mbadala cha kuhamia basi ni Chadema,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles