23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kauli ya JPM bado yazunguka kichwani kwa Makonda

NA BRIGHITER MASAKI

KAULI ya Rais Dkt. John Magufuli, kwamba kumekuwapo uzembe katika utekelezaji wa baadhi ya miradi, imeendelea kumnyima usingizi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, baada ya juzi kutembelea kwa mara nyingine mradi wa machinjio ya Vingunguti.

Makonda aliutembelea mradi huo ikiwa ni mara yake ya tano kufanya hivyo tangu kauli ya Rais aliyoitoa Septemba 16, alipofanya ziara ya kushtukiza katika machinjio hayo, akieleza kushtushwa na kukwama kwa mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa akiwataka viongozi kuhakiksiha wanafuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Wilaya ya Ilala, Makonda alisema anaridhishwa na maendeleo ya ujenzi  wa machinjio hayo.

“Nilipanga ofisini kwangu kwamba Oktoba ni mwezi wa kufuatilia miradi yetu yote mara kwa mara ili kila hatua inayofanyika tuweze kuiona na kama kuna sehemu watu wamekwama tusaidiane, tunataka tutimize miradi kwa haraka, watu wafaidike.

“Nimeridhishwa na ujenzi unaoendelea kwa sasa, utakaosaidia kusafisha na kuosha ng’ombe na nyama usiku na mchana…” alisema.

Wakati huo huo,  Mkuu wa Mkoa huyo akiwa Buguruni ambako alikagua mifereji ya Kata visiwani,  alisema amechoshwa na viongozi wanaompelekea taarifa za uongo, wakidai miradi inaendelea vizuri, wakati hali ni tofauti, akisema huo ni sawa na utapeli.

Makonda amewapa siku sita watumishi wa Tamisemi wanaohusika na miradi ya DMDP kuhakikisha miradi ya ujenzi wa mifereji inaanza na ametishia kufanya maandamano endapo watakaidi.

Aidha, Makonda ameelekeza Watumishi wa Tamisemi wanaohusika na miradi ya ujenzi wa mifereji na mito kupitia DMDP kuhakikisha kabla ya Oktoba 10 mwaka huu miradi yote ya ujenzi wa mifereji Wilaya ya Ilala iwe imeanza na endapo watakaidi ataitisha maandamano ya wakazi wa kata tano kwenda wizara ya Tamisemi.

May mwaka huu Makonda aliagiza mfereji wa Kisiwani Kata ya Buguruni ufanyiwe maboresho kutokana na kuwa chanzo cha mafuriko kwenye makazi ya watu lakini ameshangazwa kuona hakuna chochote kilichofanyika licha ya mkataba kusainiwa tangu Julai mwaka huu.

Jambo hilo lilimlazimu Makonda kumpigia simu Mratibu wa Miradi ya DMDP, Emmanuel Ndyamkana ambae alijitetea kuwa miradi hiyo inakwama kutokana na wizara ya fedha kuchelewa kutoa fedha jambo ambalo Makonda amesema ni uzembe.

Aidha Makonda ameitaja baadhi ya mifereji na mito inayotakiwa kufanyiwa maboresho ni pamoja mfereji wa Tabata kanisa la Katoliki, mfereji wa Kiwalani na baadhi ya mito yenye urefu wa Km 19 ambayo ujenzi wake utagharimu takribani Sh bilioni 32.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles