28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Katwila awapa Simba Kihimbwa

Na ZAINAB IDDY

DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuber Katwila, amesema kuwa kama Simba inamhitaji kweli mchezaji wao, Salum Kihimba, waende wakamchukue, kwani ni mmoja wa wachezaji makini na wanaojitambua.

Akizungumza na MTANZANIA, Katwila alisema kumekuwa na taarifa nyingi zinazoenea juu ya mabingwa watetezi wa ligi kumhitaji mchezaji wao na yeye kama mkuu wa benchi la ufundi hawezi kumzuia.

“Mtibwa siku zote inatoa wachezaji wazuri na wanaojitambua, mfano mzuri hao waliotangulia kucheza Simba, hivyo hata kama kweli Simba inamhitaji Kihimbwa waje tu wamchukue.

“Muangalie Hassan Dilunga, Kichuya na wengine wengi awaliotoka kwetu kwenda Simba, wameonyesha uwezo mzuri kiasi cha hivi sasa kutegemewa katika timu ya taifa ‘Taifa Stars’.”

Katwila aliongeza: “Niwashauri Simba tu, lazima wafanye mawasiliano na viongozi wa juu wa Mtibwa Sugar na si kuleta ujanja ujanja kama inavyokuwa miaka iliyopita.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles