32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

KATUMBI APINGA SERIKALI KUMZUIA

LUBUMBASHI, DRC


MWANASIASA kutoka kambi ya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi, amepinga amri ya Serikali ya Rais Joseph Kabila ya kumpiga marufuku kurudi kwake nchini DRC kutoka uhamishoni Afrika Kusini, kwakuwa ni kinyume cha haki za binadamu.

Gavana huyo wa zamani wa Jimbo la Katanga alipanga kurudi nchini mwake akipitia mjini Lubumbashi, ili kuchukua fomu ya kuwania katika uchaguzi wa urais, lakini hajapewa ruhusa ya ndege yake kutua katika ardhi ya DRC.

Vyombo vya habari nchini DRC vimeripoti kuwa, Moise Katumbi na washirika wake wanaonekana kupuuzia marufuku ya serikali hiyo, lakini ndege yake binafsi haijapewa ruhusa ya kutua.

Katika barua yake, Meya wa Jiji la Lubumbashi, Ghislain Robert Lubaba Buluma, amesema ndege ya Moise Katumbi imekataliwa kutua au kupaa katika anga ya DRC.

Duru za habari zinaeleza kuwa, Ofisi ya Mashitaka ilitangaza kwamba Moise Katumbi atakamatwa mara baada ya kuwasili nchini DRC kwa kosa la kuhatarisha usalama wa taifa.

“Moise Katumbi anakabiliwa na mashitaka ya kuajiri askari mamluki kwa lengo la kuangusha utawala wa Rais Joseph Kabila,” vyanzo kadhaa vya serikali vimeeleza.

Hatua hiyo imewashangaza wanasheria wa mwanasiasa huyo, ambao wamesema kesi hiyo ilikuwa ikisubiriwa kusikilizwa baada ya kukata rufaa.

“Ofisi ya mashitaka imeharakisha kutangaza hatua hiyo wakati ambapo hakuna sababu ya mteja wetu kukamatwa. Tumesikia kuhusu tishio hili la kukamatwa. Tuko katika nchi ya sheria, kukamatwa kufanyika kufuata sheria na utaratibu,” amesema Jean-Joseph Mukendi, mratibu wa muungano wa wanasheria wa Katumbi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles