27.5 C
Dar es Salaam
Sunday, December 3, 2023

Contact us: [email protected]

Katibu wa AMCOS Maswa kortini kwa uhujumu uchumi

Na Samwel Mwanga, Maswa

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) imemfikisha Katibu Wa Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS) cha Mbaragane katika Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Samwel Makeja katika mahakama ya wilaya hiyo kwa makosa mawili ya Uhujumu Uchumi.

Katibu huyo amesomewa mashtaka hayo leo Ijumaa Juni 17, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa, Chirstian Rugumila.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashtaka Takukuru, Albert Mwingilwa, mshtakiwa alitenda makosa hayo Oktoba 4, 2021 katika Wilaya ya Maswa ambapo alifanya ubadhilifu pamoja na kuchepusha fedha.

Mwendesha Mashtaka huyo aliendelea kuieleza mahakama kuwa kosa la kwanza ni kwamba mshitakiwa akiwa Katibu wa Amcos ya Mbaragane alifanya ubadhilifu Sh 2,000,000 ambazo alipaswa kulipia ushuru wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU) katika msimu wa ununuzi wa pamba wa mwaka 2021/2022.

“Kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 28 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura 329 marejeo ya mwaka 2019.

“Katika kosa la pili mshtakiwa alichepusha fedha hizo kwa madhumuni yake binafsi kinyume na kifungu  cha 29 cha sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya Mwaka 2019,” amedai Mwingilwa.

Mshitakiwa mara baada ya kusomewa mashitaka hayo aliyakana na hivyo kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24, mwaka huu itakaporudi kwa ajili ya kusomewa hoja za awali kwani upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles