22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Katibu, Mweka hazina CWT kizimbani kwa kuchepusha milioni 13.9

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Deus Seif na Mweka Hazina wa chama hicho, Abubakar Allawi wamepanda kizimbani wakituhumiwa kwa mashtaka mawili ikiwemo kuchepusha Sh milioni 13.9.

Washtakiwa hao wamepanda kizimbani leo saa nane mchana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rashid Chaungu.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali kutoka Takukuru, Imma Nitume alidai katika shtaka la kwanza Kati ya Oktoba 3 na Novemba 6 mwaka 2018, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa CWT walitumia madaraka vibaya na kujipatia Sh 13,930,963.

Katika shtaka la pili wanadaiwa katika kipindi hicho CWT Kinondoni wakiwa waajiriwa walichepusha kiasi hicho cha fedha mali ya Chama cha Walimu.

Washtakiwa wameshtakiwa kwa Uhujumu Uchumi lakini Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuruhusu washtakiwa kujibu mashtaka.

Kutokana na hati hiyo Washtakiwa waliruhusiwa kujibu mashtaka ambapo wote walikana, Mahakama ilikubali kuwapa dhamana kwa masharti ya kuwasilisha fedha taslim Sh 3,482,740 au umiliki wa mali isiyohamishika.

Pia wametakiwa kuwa na mdhamini mmoja kila mmoja atakayesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni 7.

Washtakiwa walikubali kuwasilisha zaidi ya Sh milioni tatu na mdhamini mmoja.

Wakili Nitume alidai upelelezi umekamilika kesi itakapokuja kwa tarehe itakayopangwa washtakiwa watasomewa maelezo ya awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles